WANANCHI WA BUKONDAMOYO WILAYANI KAHAMA WAUNGANA KUTENGENEZA MITARO YA BARABARA

Image result for PICHA WANANCHI WAKIJENGA MITARO
Na Ndalike Sonda
KAHAMA.

Wananchi wa Kitongoji cha Mlimani Katika Mtaa wa Bukondamoyo, Kata ya Mhungula Mjini KAHAMA kwa pamoja wameungana kutengeneza barabara kwa kujenga mitaro na kumwaga vifusi katika maeneo korofi ili kupata barabara ya uhakika inayofika hadi kwenye makazi yao.

Wakizungumza leo na KAHAMA FM, baadhi ya wananchi hao, wamesema wameamua kutengeneza barabara hiyo baada ya eneo la shule kupandwa miti na hivyo kuwa na usumbufu mkubwa wa barabara inayounganisha kitongoji hicho na barabara kuu inayokwenda mjini Kahama.

Wananchi hao, JENNY GINDON, PETER MASANJA, na SELESTINA MICHAEL mbali na kujitolea kutengenza barabara hiyo, wameiomba serikali kuwasaidia kuboresha barabara hiyo kwa kuweka makaravati yatakayosaidia kupitsisha maji yanayotoka Mlimani.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Bukondamoyo, NASHON YOHANA amesema Kukamilika kwa barabara hiyo itasaidia kupunguza adha wanayoipata kwa sasa wananchi wa mtaa huo, na kwamba hadi sasa wananchi wamechangia zaidi ya shilingi laki tano kwaajili ya kuboresha barabara hiyo.

Hii ni mara ya Pili kwa wananchi wa Mtaa wa Bukondamoyo kujitolea kutengeneza barabara ambapo hivi karibuni walishiriki kumwaga vifusi vya changalawe kwenye karavati lililopo Kitongoji cha Pugu katika mtaa huo ili kuunganisha mawasiliano ya barabara.
Share:

HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA KUGAWA VYANDARUA VYENYE DAWA KWA WANAWAKE NA WATOTO WANAOFIKA KLINIKI


Na Ndalike Sonda
KAHAMA.

Halmashauri ya Mji wa KAHAMA imeanzisha utaratibu wa kugawa vyandarua vyenye dawa kwa wanawake na watoto wanaofika klinik katika hospitali ya Halmashauri hiyo ili kuhamasisha matumizi ya vyandarua na hivyo kupunguza vifo vitokanavyo na Ugonjwa wa malaria.

Akizungumza kwenye kipindi cha Raha ya Leo, cha KAHAMA FM, kaimu Mratibu wa Malaria wa halmashauri hiyo Dkt. HEMED BIHEMO amesema utaratibu huo umetokana na ongezeko la ugonjwa huo katika halmashauri hiyo.

Amesema, kipindi cha kuanzia mwezi Disemba 2017 hadi April Mwaka huu, Halmashauri hiyo ikuwa na asilimia 31 ya wagonjwa wa malaria ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana ambayo ilikuwa ni asilimia 25.

Dkt. BIHEMO amesema kundi la watoto na wanawake wajawazito ndio wameonekana kuongoza kuugua ugonjwa huo na kwamba idadi hiyo inatokana na makundi hayo kuwa tayari kupima ugonjwa huo tofauti na wanaume ambao wamekuwa hawafanyi vipimo.

Halmashauri ya mji wa Kahama inajumla ya vituo 13 vya umma na 21 vya binafsi vinavyotumika kupima ugonjwa huo idadi ambayo inatajwa kuwa ni ndogo ikilinganishwa na wingi wa watu katika halmashauri hiyo.
Share:

KIJANA ANAYEDHANIWA KUTAPELI NYAMA BUCHANI ANUSURIKA KIFO


Na Ndalike Sonda
KAHAMA.

Mkazi wa Nyahanga Mjini KAHAMA RAMADHAN HAMIS (36) amenusurika kuuawa na wananachi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuiba nyama katika chucha Moja iliyopo Mtaa wa Nyahanga.

Tukio hilo hilo limetokea leo majira ya saa tatu asubuhi ambapo RAMADHAN anadaiwa kufika katika bucha hiyo na kuomba apimiwe nusu kilo ya Nyama yenye thamani ya Shilingi 3000.

Akizungumza na KAHAMA FM, Muuzaji wa bucha Hiyo JOHN JOSEPH amesema Mtuhumiwa (RAMADHAN) huyo alifika katika bucha hiyo na kumwambia kuwa ampimie kiasi hicho cha nyama ili ampeleke kwenye hoteli ya mke wake iliyopo jirani na bucha hiyo ambapo pia aliomba pesa aifuate hapo.

Alisema baada ya kumpimia Nyama mtuhumiwa (RAMADHAN) alikwenda kwenye hoteli hiyo na kisha kutoka pasipo kulipa ambapo alimuomba alipe pesa hiyo kama alivyoahidi ambapo alianza kukimbia na ndipo wananchi walipoanza kumfukuza na kisha kumkamata.

Naye RAMADHAN ambaye ni Mtuhumiwa amesema amekuwa akienda akukopa kwenye bucha hiyo kwa kutokana na muuzaji wa zamani aliyemuita MURA, hivyo ni kama mazoea kwake kwenda pale kukopa na kulipa baadaye.

Mmoja wa Mashuhuda ERIC JOHN ambaye anaegesha pikipiki eneo hilo, amesema hajawahi kumuona katika eneo hilo mtuhumiwa huyo na kwamba alifika asubuhi akanunua pombe ya shilingi 1000, katika duka moja lililopo eneo hilo ambapo baada ya kudaiwa pesa aliamua kuacha simu yake kama mdhamana.

Hata hiyo wanawake wanauza hoteli katika eneo hilo wamesema hawamjui mtuhumiwa huyo na kwamba alifika hapo kisha kuondoka huku akiwaambia kuwa ni fundi ujenzi ambapo kunavijana wake watakuja kunywa chai baadaye.

Hata hivyo msamaria Mmoja alimlipia kiasi hicho cha fedha kwenye bucha hiyo pamoja na kwenye duka analodaiwa kisha wananchi wakamuachia akaenda zake.

Share:

JESHI LA POLISI MKOANI SHINYANGA LAENDELEA KUFANYA UCCHUNGUZI WA MAUAJI YA SHOMA MWENYE UMRI WA MIAKA 70

Na Sebastian Mnakaya
SHINYANGA.

Jeshi la polisi mkoani SHINYANGA, linaendelea kufanya uchunguzi katika tukio la mauaji ya mwanamke aitwaye, SHOMA SHIJA mwenye umri wa miaka 70 yaliyotokea juzi katika kijiji cha Shabuluba kata ya Busanda wilaya ya Shinyanga pamoja na vifo vingine vya watu wawili.

Kamanda wa polisi wa Mkoa huo, SIMON HAULE amewaambia wandishi wa habari kuwa tukio hilo limetokea juzi usiku wakati marehemu SHOMA akiwa nyumbani kwake ambapo alivamiwa na watu ambao idadi yao haikuweza kufahamika.

Katika tukio lingine lililotokea jana asubuhi katika mtaa wa Muhungula mjini Kahama, Kamanda HAULE amesema, mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Nyahanga, DANIEL YOHANA MAZIKU mwenye miaka 9 amegundulika akiwa amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye karo.

Kamanda HAULE ameongeza kuwa katika manispaa ya Shinyanga mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mwasele aliyetambulika kwa jina la HAPPINESS amegundulika amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba aliyoifunga katika dari la nyumba aliyokuwa anaishi na wazazi wake.

Kamanda HAULE ametoa rai kwa wazazi na walezi kuchukua tahadhari kubwa ya kuwatunza, kuwalinda na kuwafuatilia watoto wao hususan katika kipindi hiki cha msimu wa mvua.

Amesema jamii ni vizuri pia ikawa karibu na watoto na vijana ili kujua shida na changamoto zinazowakabili ili kuchukua hatua za kuwashauri na kuwatia moyo wa matumaini pale wanapokata tamaa ya maisha.

Share:

WAFANYABIASHARA WA SOKO LA NAMANGA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA WAPO HATARINI KUKUMBWA NA MLIPUKO WA MAGONJWA

Image result for WAFANYABIASHARA WALIO KATIKA HALI MBAYA
Na Ndalike Sonda
KAHAMA.

Wafanyabiashara na wananchi waliopo katika soko la Namanga Mjini KAHAMA wapo hatarini kukumbwa na mlipuko wa magonjwa kutokana na kukithiri kwa mlundikano wa taka katika milango ya kuingia na kutoka sokoni hapo.

Wakizungumza kwenye kipindi cha Raha ya leo, Baadhi ya wafanyabiashara na wananchi wamesema harufu mbaya imekuwa ikitoka katika uchafu huo na kwamba hali hiyo inatokana na uchafu huo kuchukua muda mrefu pasiko kuzolewa.

Kutokana na hali hiyo wameiomba serikali kuingilia kati, ili kudhibiti mlundikano wa uchafu huo na kwamba imekuwa ni kero kwa wananchi waishio jirani na soko hilo pomoja na wanafunzi wa shule ya Msingi Kilima A na B.

Mmoja wa viongozi wa katika Eneo hilo (NZENGO), HAMIS SAID amesema wamekuduia kuandika barua kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Kahama ili kumuomba afike eneo hilo kujionea hali halisi.

Naye Katibu wa Soko la Namanga, WILLIUM CHALYA amesema uchafu huo umekaa zaidi ya wiki mbili na kwamba wameweka ulinzi ili kudhibiti wananchi wasiendelee kutupa taka eneo hilo.

Soko la Namanga ni Soko linalohudumia idadi kubwa ya watu katika halmashauri ya mji wa Kahama kwa sasa ambapo lina zaidi ya wafanyabishara 1500 wanaofanya biashara zao ndani ya soko hilo.
Share:

WANANCHI WA HALMASHAURI YA MSALALA WILAYANI KAHAMA WATAKIWA KUJIANDAA NA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Image result for VITAMBULISHO VYA TAIFA
Na Salvatory Ntandu
KAHAMA.

Serikali Wilayani KAHAMA imewataka wananchi wa Halmashauri ya Msalala Wilayani wilayani humo kujiandaa na zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa linalotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, FADHILI NKURLU wakati akizungumza na waandishi wa Habari mjini Kahama kuhusiana na namna zoezi hilo litavyotekelezwa na kusema kuwa Halmashauri ya mji wa Kahama inaelekea kuhitimisha zoezi hilo hivi karibuni.

Amesema zoezi hilo linatekelezwa na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) na linafanyika bure na hakuna mwananchi atakayetozwa gharama yeyote hivyo wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.

Amefafanua kuwa Mpaka sasa Halmashauri ya Mji wa Kahama imeandikisha watu elfu 99 na 750 sawa na asilimia 87 ya lengo liliowekwa la kuandikisha watu laki 1 na 14 elfu 260.
Share:

SHULE ZA MSINGI TATU ZAFUNGWA WILAYANI KAHAMA KWA AJILI YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

Image result for SHULE ZILIZOJAA MAJI
Na Amina Mbwambo
KAHAMA.

Kamati ya Maafa ya wilaya ya KAHAMA mkoani Shinyanga imelazimika kuzifunga shule tatu za msingi katika kata ya Jana Halmashauri ya Msalala baada ya kuzungukwa na maji kufuatia mvua kubwa zilizonyesha sehemu mbalimbali wilyani humo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kahama, FADHILI NKURLU amesema wamelazimika kuifunga shule ya Izuga yenye wanafunzi 525, Kadati yenye wanafunzi 348 na Matindye yenye wanafunzi 355 kuanzia kesho Aprili 19 hadi Aprili 30, mwaka huu.

NKURLU amesema katika Halmashauri ya Ushetu watu wanne wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba katika kijiji cha Mbika, huku nyumba 74 zikibomolewa katika kata ya Uyogo na daraja kusombwa na maji katika kata ya Bulungwa.

Taarifa zaidi kutoka halmashauri ya Ushetu zinabainisha kuwa mawasiliano ya barabara kati ya mji wa Kahama na kata za Ulewe, Nyankende na Ubagwe kupitia kata ya Bulungwa katika Halmashauri hiyo, yamekatika kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo.

Akiongea na Kahama fm kutoka Bulungwa, mkazi wa mjini Kahama, MARCO MIPAWA ambaye ni miongoni mwa watu walioshindwa kusafiri kufuatia mvua hizo, amesema daraja la Kabanga katika kata ya Sabasabini, Halmashauri ya Ushetu limefunikwa maji na kusababisha magari kushindwa kupita.

Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa wilaya ya Kahama, NKURLU wameuagiza wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA), kuchukua hatua za haraka kuhakikisha mawasiliano yanarejea, huku akiwasihi Wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya mvua zinazoendelea kunyesha kuepuka madhara.
Share:

ASKARI WA JWTZ ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA YA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI BBAADA YA KUWAGONGA NA GARI.


Na Salvatory Ntandu
KAHAMA.

Mkazi wa Old Shinyanga mkoani SHINYANGA, PHINEHAS CHOGELO (29) ambaye pia ni Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa Tuhuma ya kusababisha vifo vya watu wawili baada ya kuwagonga kwa gari.

Kwa Mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa SHINYANGA SIMON HAULE, tukio hilo limetokea Aprili 8 mwaka huu, majira ya saa tano asubuhi katika eneo la Ibinzamata barabara itokayo Shinyanga mjini kuelekea Tinde, Shinyanga vijijini.

Amesema gari T. 105 DGQ Subaru Forester likiendeshwa na CHOGELO liliigonga pikipiki aina ya San Lg namba za T. 974 BSL iliyokuwa ikiendeshwa na YAHYA NASORO(36) mkazi wa Kitangili aliyekuwa amempakia CATHERINE MWIGULU(35) mkazi wa Nhelegani na kuwavunja miguu yao ya kulia.

Amefafanua kuwa CHOGELO pia alimgonga mwendesha baiskeli STEVEN JOSEPH(25), mkazi wa Isela aliyekuwa amempakia NEMEM JOSEPH(26) mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi Kolandoto, na kusababisha vifo vyao wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Kamanda HAULE amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari husika na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi na vielelezo vipo kituoni.

Share:

AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI SITA AU KULIPA FAINI KWA KOSA LA KUWEPO NCHINI KINYUME CHA SHERIA



Na Paulina Juma
KAHAMA.
 
Raia wa Burundi, NSABIMANA RAMADHAN (23) amehukumiwa kwenda jela miezi 6 au kulipa faini ya shilingi 500,000 kwa kosa la kuwepo nchini kinyume na sheria ya uhamiaji.

Huku hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya KAHAMA IMANI BATENZI, baada ya NSABIMANA kukiri kutenda kosa hilo.

Awali mwendesha mashitaka wa Idara ya Uhamiaji, SALUMU RASHID amesema RAMADHAN alikamatwa April 10 mwaka huu maeneo ya Soko kuu mjini Kahama akiwa hana kibali kinachomruhusu kuwepo nchini.

Katika shauri hilo la jinai namba 149/2018, RAMADHAN ametenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 45 cha sheria ya uhamiaji namba 7 ya mwaka 1995 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016.

RAMADHAN ameshindwa kulipa faini na ameanza kutumikia kifungo cha miezi 6 jela na mara baada ya kumaliza kifungo hicho atarejeshwa nchini kwao Burundi.
Share:

WAKAZI WA MALUNGA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA WALALAMIKIA UBOVU WA KARAVATI LILILOPO JIRANI NA OFISI YA KATA


Na Ndalike Sonda
KAHAMA.

Wananchi wa kata ya Malunga katika Halmashauri ya Mji wa KAHAMA Mkoani SHINYANGA wamelalamikia ubovu wa karavati lililopo jirani na ofisi ya Kata hiyo kutokana na kuchimbuliwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi ya mji wa Kahama.

Wakizungumza kwenye kipindi cha Raha ya Leo cha KAHAMA FM, baadhi ya wananchi wamesema kutokana na ubovu wa barabara hiyo kwa sasa ajali nyingi zimekuwa zikitokea ikiwamo magari kuzama na kusababisha msongamano mkubwa wa watumiaji wa barabara hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Korogwe katika kata hiyo ya Malunga, EDWARD MBELELE amekiri kushuhudia ajali mbili katika eneo hilo kwa kuwa ni jirani na ofisi yake ambapo amesema suala hilo wamelifikisha kwenye kikao cha maendeleo ya kata (WDC).

Meneja wa wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) katika halmashauri ya Mji wa Kahama, JOB MUTAGWABA amekiri kupokea taarifa ya ubovu wa karavati hilo na kwamba wako katika hatua ya kulirekebisha.

Aidha amesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika wilaya ya Kahama, barabara nyingi zimeharibika na kwamba wanakusudia kuziimarisha baada ya masika kumalizika na kuwataka wananchi wawe na subira.
Share:

SERIKALI YASEMA BADO KUNA UTOROSHAJI MWINGI WA DHAHABU MIGODI YA SHINYANGA



Na Ndalike Sonda
KAHAMA.

Serikali imesema bado kuna utoroshaji mwingi wa dhahabu katika machimbo madogo Mkoani SHINYANGA hali inayosababisha serikali kukosa mapato mengi ambayo yangesaidia kuboresha huduma mbalimbali za jamii.

Hayo yameelezwa Mjini KAHAMA na Naibu waziri wa Madini, DOTTO BITEKO wakati akizungumza na wachimbaji na wachenjuaji wa madini wa mkoa wa Shinyanga kwenye semina ya kujadili usalama mahala pa kazi.

Amesema kuanzia mwezi June 2016 hadi Februari mwaka huu, wachimbaji wadogo mkoani Shinyanga wamezalisha kilo 555.7 za dhahabu (sawa na shilingi milioni 45), kiwango ambacho amesema kipo chini ukilinganishwa na uzalishwaji.

BITEKO amesema wachimbaji wa madini wanazidiwa na wachimbaji wa kokoto na mchanga ambao mwaka jana wamechimba tani milioni 15 na kulipa mrabaha shilingi wa biloni 7.5 serikalini.

Wakizungumza na waandishi wa Habari baadhi ya wachimbaji na wachenjuaji wameshauri kuongezwa udhibiti dhidi ya utoroshaji madini hayo pamoja na kupunguza tozo na kodi mbalimbali kwa wachimbaji wadogo kwa manufaa ya serikali na wachimbaji hao.
Share:

WANANCHI WALIOVAMIA ENEO LA MGODI WA ACACIA BULYANKULU WAAMRIWA KUONDOKA


Na Salvatory Ntandu
KAHAMA.

Zaidi ya wachimbaji wadogo wa madini 800 waliovamia eneo linalomilikiwa na mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyankulu katika Halmashauri ya Msalala, Wilayani Kahama wameamriwa kuondoka katika eneo hilo mara moja.

Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Kahama FADHILI NKURLU wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na namna zoezi hilo litakavyotekelezwa.

Amesema ingawa ramani inaonesha kuwa eneo hilo liko ndani ya leseni ya Acacia mkazi mmoja alijenga nyumba katika eneo hilo kwa lengo la kuishi na badala yake alianza kuchimba dhahabu hali iliyosababisha wachimbaji wengine kulivamia.

Wavamizi hao wamefanya uharibifu mkubwa wa ardhi kwa kuchimba mashimo mengi ambayo kwa mujibu wa NKURLU ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kahama yatafukiwa kesho ili kuzuia madhara kwa binadamu.
Share:

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI KINYUME CHA SHERIA


Na Lilian Katabaro
KAHAMA.

Raia wa Rwanda, NIYOMUGABO PASIFIQUE (21), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya KAHAMA kwa tuhuma ya kuingia na kuwepo nchini kinyume cha sheria.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo IMANI BATENZI, mwendesha mashitaka wa Idara ya ya Uhamiaji SALUM RASHIDI, amesema NIYOMUGABO alikamatwa March 6 mwaka katika mtaa wa Mwime wilayani Kahama akiwa hana kibali kinachomruhusu kuwepo nchini.

SALUM amesema katika shauri hilo la jinai namba 146/2018, NIYOMUGABO ametenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 45 na kifungu cha pili cha sheria ya Uhamiaji namba 7 ya mwaka 1995 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016.

NIYOMUGABO amekana kutenda kosa hilo na upelelezi wa shauri hilo umekamilika na hoja za awali zitasikilizwa Mahakamani hapo April 10 mwaka huu na amerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
Share:

GULIO LA MHULIDEDE USHETU WILAYANI KAHAMA KUFANYIWA MAREKEBISHO.


Na Ndalike Sonda
KAHAMA.

Uongozi wa Kata ya Igunda Halmashauri ya USHETU wilayani KAHAMA Mkoani SHINYANGA umeahidi kuendelea kuweka miundombunu rafiki kwenye gulio la Kijiji cha Mhulidede ili wafanyabiashara na wananchi walitumie bila kupata adha yoyote.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa soko hilo Diwani wa Kata ya Igunda, TABU KATOTO amesema wataongeza msukumo wa kupeleka huduma muhimu katika gulio hilo huku Kaimu Afisa Mtendaji wa kata hiyo EVODIUS MWESIGE, akiwataka wananchi kutumia gulio hilo kujiimarisha kiuchumi.

Nao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mhulidede, wameipongeza serikali ya kijiji hicho kwa kuweka gulio ambalo litawasaidia kubuni biashara mbalimbali za kuwaingizia kipato.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake katika gulio hilo, WILIAM JOSEPH amesema wamekusudia kujipanga ili kuomba mikopo mbalimbali kwa halmashauri ya Ushetu, kwa lengo la kujiimrisha biashara.

Gulio la Kijiji cha Mhulidede limefunguliwa rasmi leo ambapo litakuwa likifanyika kila siku ya jumatatu katika kijiji hicho.
Share:

UHABA WA VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA MSINGI NYAHANGA YAWA CHANG.AMOTO KWA WANAFUNZI


Na Salvatory Ntandu
KAHAMA.

Uhaba wa vyumba vya Madarasa katika Shule tatu za Msingi zilizopo katika Kata ya NYAHANGA, Halmashauri ya Mji wa KAHAMA huenda ukasababisha wanafunzi kutofanya vizuri katika masomo yao.

Hayo yamebainishwa jana na diwani wa Kata hiyo, MICHAEL MAGILE wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara kuhusiana na namna watakavyojipanga kutatua tatizo hilo kwa kuchangia.

Amesema endapo wananchi watakubali kuchangia maendeleo ya shule kwa hiari wataweza kujenga vyumba vya madarasa vya kutosha na kumaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa katika kata hiyo.

Awali akiwasilisha taarifa ya shule hizo, Afisa elimu kata ya Nyahanga HELENA KABOYA amesema kata hiyo inaupungufu wa vyumba vya madarasa 81 kwa shule zake tatu ambazo ni shule ya Msingi Nyahanga A,B na Shunu.

Amesema katika shule ya Msingi Nyahanga A vinahitajika vyumba vya madarasa 31 ambapo vilivyopo ni 12 na pungufu ni 19.

Amesema katika shule ya Nyahanga B vinahitajika vyumba 37 wakati vilivyopo ni 14 na upungufu ni vyumba 23, huku shule ya Shunu ikihitaji vyumba 47 vilivyopo ni 8 na pungufu ni 34.

Nao baadhi ya wananchi waoshiriki katika Mkutano huo BUNDALA SENGASENGA na SELEMAN KIJA wamesema endapo viongozi wa kata hiyo wataondoa tofauti zao binafsi, wananchi wakotayari kuchangia maendeleo ya kata hiyo.

Kata ya Nyahanga ina jumla ya shule za msingi saba ambapo tatu ni za serikali na 5 ni za binafsi
Share:

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels