Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ametoa siku saba kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Kagera (RCO), Obassy Nguvillan, kupeleleza upya kesi ya mama aliyechomewa nyumba katika eneo la Kyakailabwa Kata ya Nyanga, Manispaa ya Bukoba.
Lugola
 alitoa agizo hilo jana kutokana na watuhumiwa kukamatwa kisha kuachiwa 
na baadaye jalada kufungwa na Mwanasheria wa Serikali.
Kabla
 ya agizo hilo, mama huyo, Sauda Amir, alilalamika kwa Waziri Lugola 
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Uhuru Manispaa ya
 Bukoba na baadaye RCO alikiri kuwa inawezekana Jeshi la Polisi 
lilipeleleza kesi hiyo kwa udhaifu.
Lugola
 alisema kuwa haiwezekani mwanamke huyo achomewe nyumba, watuhumiwa 
anawafahamu halafu kesi iishe katika mazingira ambayo yana utata na 
kulazimika kumwita RCO kujibu.
“RCO natoa muda wa wiki moja ufanye kazi hii wewe mwenyewe, uchunguze kesi hii upya na unipe majibu,” alisema.
Akizungumzia
 tukio hilo, Sauda anayedai alifiwa na mumewe, alisema kuwa nyumba yake 
ilichomwa moto Juni 11, mwaka jana na kuwa kutokana na tukio hilo, kwa 
sasa hana mahala pa kuishi.
“Mheshimiwa
 Waziri, naomba unisaidie suala langu lipatiwe ufumbuzi, nahangaika na 
watoto, sina pa kuishi, kwa sasa mimi na watoto wangu saba tumepewa 
hifadhi na mama mmoja katika eneo la Kyakailabwa,” Alisema mama huyo






Va Kearney 36 months previously with U . s . https://imgur.com/a/AONoinb https://imgur.com/a/MW98GW1 https://imgur.com/a/111J9ak https://imgur.com/a/K5Xv7vg https://imgur.com/a/fkGyFec https://imgur.com/a/lwmIUZF https://imgur.com/a/vQRgsmr
ReplyDelete