WATU WANNE WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAUAWA NA POLISI


Na Salvatory Ntandu
KAHAMA.

Watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuawa katika majibizano ya risasi baina yao na askari polisi katika Makaburi ya Kitwana wilayani Kahama, huku silaha nne za kivita na bomu moja la kutupa kwa mkono vikipatikana katika tukio hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mjini Kahama Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, SIMON HAULE amesema tukio limetokea jana majira ya saa sita mchana baada ya watuhumiwa hao kutaka kuwakimbia polisi waliokuwa wanawashikilia.

Amesema watu hao walikamatwa na Jeshi la Polisi katika mikoa ya Tabora, Katavi, Shinyanga na Kigoma ambapo walitoa ushirikano kwa jeshi la Polisi na kuonesha Mahali ambapo huwa wanaficha silaha hizo katika eneo la Makaburi ya Kitwana.

Naye Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Shinyanga aliyeendesha msako huo, AMADIUS TESHA amewataka Majambazi popote walipo kusalimisha silaha zao na wasipofanya hivyo hawatasalimika.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kitwana wamelipongeza jeshi la Polisi kufanikisha msako huo ambao umewezesha kukamatwa kwa silaha hizo.

Silaha zilizokamatwa ni pamoja na bunduki aina ya AK47 yenye risasi 30, Shotgun 1, Bastola 2 zenye risasi na Bomu moja la kutupa kwa mkono.
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels