AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA YA KUMSABABISHIA UJAUZITO MWANAFUNZI


Na Lilian Katabaro
KAHAMA.

Mkazi wa kijiji cha Ufala Wilayani KAHAMA, JOSHUA ANDREW amefikishwa katika mahakama ya Wilaya hiyo kwa tuhuma ya kubaka na kumsababishia ujauzito mwanafunzi wa miaka 16 kinyume na sheria.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, USHINDI SWALLO, Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi, FELIX MBISE amesema ANDREW alitenda kosa May 31 mwaka huu saa 2 asubuhi katika kijiji cha Ufala ambapo alimbaka mwanafunzi huyo na kumsababishia ujauzito.

FELIX amesema katika shauri hilo la jinai namba 215/2018 ANDREW anatuhumiwa kwa kosa la kwanza la kubaka kinyume na kifungu 130 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Amesema kosa la pili, ANDREW anatuhumiwa kumsababishia mwanafunzi ujauzito kinyume na kifungu namba 60 A cha sheria ya elimu sura ya 353 kanuni ya adhabu ya mwaka 2016.

ANDREW amekana kutenda kosa hilo na upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na shauri hilo litatajwa tena mahakamani hapo June 23 mwaka huu na amerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels