KAHAMA.
Wakazi watatu wa kijijini cha MTAKUJA na mmoja mkazi wa NYANTAKARA wilaya ya Bukombe mkoani Geita wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama kwa tuhuma ya kuingia katika hifadhi ya pori la Moyowosi Kigosi kinyume cha sheria.
Waliofikishwa mahakamani ni pamoja na YUSUPH DANIEL (58), ISURURU KAGEMBE (64), NTEMI MASASILA (36) na SAFARI LUCAS (21) mkazi wa Nyantakara Bukombe mkoani Geita.
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo USHINDI SWALLO mwendesha mashitaka wa Idara ya wanyama pori CATHELINE ALOYCE amesema washitakiwa walitenda kosa hilo June 15 mwaka huu majira ya saa 11 jioni ambapo waliingia ndani ya hifadhi bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori.
CATHELINE amesema washitakiwa hao pia waliharibu uoto wa asili ndani ya hifadhi hiyo kwa kukata miti kwa ajili ya mbao bila kibali kutoka kwa mkurungezi wa wa wanyamapori.
Katika shauri hilo la jinai namba 223/2018 Washitakiwa wote wamekili kutenda kosa la kuingia hifadhi kinyume na kifungu namba 15 cha sheria ya uhifadhi wanyama pori namba 5 ya mwaka 2009.
Hata hivyo hoja za msingi zitasomwa Mahakamani hapo June 29 mwaka huu na watumiwa wote wamerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
No comments:
Post a Comment