WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUINGIA PORI LA AKIBA LA KIGOSI MOYOWOSI KINYUME CHA SHERIA


Na Lilian Katabaro
KAHAMA.

Wakazi wa kijijini cha Kilimahewa wilayani Kahama EZEKIEL CHARLES (52) na REVOKATUS MAGANGA (36) wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya hiyo kwa tuhuma za kuingia katika Pori la Akiba la Moyowosi-Kigosi na kupatikana na mchanga wenye madini bila kibali.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo IMANI BATENZI, mwendesha mashitaka wa Idara ya wanyama pori CATHERINE ALOYCE amesema washitakiwa walitenda kosa hilo Mei 30 mwaka huu majira ya saa nne usiku kwa kuingia ndani ya hifadhi bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori.

CATHERINE amesema katika shitaka la pili washitakiwa hao pia walikamatwa wakiwa na mchanga unaosadikika kuwa na madini ya dhahabu viroba vinne kinyume na kifungu namba 20 cha sheria ya uhifadhi wanyama pori ya mwaka 2009.

Katika shauri hilo la jinai namba 206/2018 Washitakiwa wamekiri kuingia katika Pori hilo la Akiba Moyowosi-Kigosi kinyume na kifungu namba 15 cha sheria ya uhifadhi wa wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.

Kosa la pili ni kupatikana na mchanga unaodhaniwa unamadini ya dhahabu kinyume na kifungu namba 20 cha sheria ya uhifadhi wanyamapori ya mwaka 2009.

Kufuatia hatua ya Washitakiwa kukiri makosa hayo, hoja za msingi zitasomwa Mahakamani hapo June 14 mwaka huu na watuhumiwa wote wamerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels