JESHI LA POLISI JIJINI DODOMA LAKAMATA WATUHUMIWA AKIWEMO CHIDI BENZI

Image result for kamanda mkuu dodoma
Na Lilian
DODOMA

Jeshi la polisi Mkoani DODOMA limemtia Mbaroni mtuhumiwa wa kosa la mauji ya mhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma UDOM pamoja na watuhumiwa wengine 7 akiwemo msanii wa muziki wa bongo fleva RASHID ABDALLAH Maarufu CHID BENZI kwa kosa la kujihusisha na biashara haramu.

Akizungumza na waandisha wa habari kamanda wa polisi mkoani Dodoma GILLES MUROTO Amesema jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa aliyehusika na mauji ya Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma UDOM ROSE MALFRED MDENYE na mume wake JOHN MWAISAGO yaliyotokea tarehe 25.05.2018 swaswa mtaa wa sulungai na mtuhumiwa huyo kutororka.

Mtuhumiwa huyo ametiwa baroni akiwa mafichoni katika kijiji cha chiwachiwa kata ya mbigu wilaya ya ifakara mkoani Mororgoro na atafikishwa mahakamani kwa kosa la kuua kwa kukusudia.

Kupitia operesheni hiyo ya jeshi la polisi msanii wa mziki wa bongo fleva ABDALLAH RASHID (33) Maarufu kama CHID BENZ amekamatwa akiwa na Bhagi gram 5 katika msokoto ambayo ni kinyume cha sheria na mtuhumiwa huyo atafikishwa tena mahakamani kwa kosa jipya.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine saba 7 katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Tanzania wakijihusisha na biashara haramu ya wanyamapori ambao ni kombe 536 ikiwa ni kinyume cha sheria.

Kwa upande wake afisa wanyamapori mkoa wa Dodoma SLIVANUS OKUDO mewaomba wananchi kufikisha taarifa pindi wanapoona wahujumu wa maliasili na kupeleka nje ya nchi ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

Jeshi la polisi limewatahadharisha wananchi kuacha kujihusisha na masuala ya uhalifu kwani mkondo wa sheria utafanya kazi yake
Share:

BAADHI YA WANANCHI WA KAHAMA WATOA MAONI YAO JUU YA BAJETI INAYOENDELEA KUJADILIWA BUNGENI DODOMA

Image result for bajeti ya tanzania 2018/19
Na Leah Samson
KAHAMA.

Baadhi ya wananachi Wilayani KAHAMA Mkoani SHINYANGA wamesema bajeti ya fedha ya mwaka 2018/2019 inayoendelea kujadiliwa bungeni Mjini Dodoma, huenda ikatoa fursa ya maendeleo kwa wananchi na taifa kutokana na kuwa imegusa maisha ya Watanzania walio wengi.

Wakizungumza na Kahama fm, wananachi hao wamesema wameipokea vizuri bajeti hiyo iliyowasilishwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Waziri wa Fedha na Mipaango Dokta PHILIPH MPANGO hasa katika suala la kutokuongeza kodi kwenye bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi.

Katika hatua nyingine wananchi hao pia wametoa wito kwa serikali kuongeza bajeti ya kilimo kwani asilimia kubwa ya wanchi nchini wanategemea sekta hiyo katika kujiimarisha kiuchumi.
Share:

WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUINGIA IFADHINI KINYUME CHA SHERIA.

Image result for nyundo mahakamani
Na Paulina juma
KAHAMA.

Wakazi watatu wa kijijini cha MTAKUJA na mmoja mkazi wa NYANTAKARA wilaya ya Bukombe mkoani Geita wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama kwa tuhuma ya kuingia katika hifadhi ya pori la Moyowosi Kigosi kinyume cha sheria.

Waliofikishwa mahakamani ni pamoja na YUSUPH DANIEL (58), ISURURU KAGEMBE (64), NTEMI MASASILA (36) na SAFARI LUCAS (21) mkazi wa Nyantakara Bukombe mkoani Geita.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo USHINDI SWALLO mwendesha mashitaka wa Idara ya wanyama pori CATHELINE ALOYCE amesema washitakiwa walitenda kosa hilo June 15 mwaka huu majira ya saa 11 jioni ambapo waliingia ndani ya hifadhi bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori.

CATHELINE amesema washitakiwa hao pia waliharibu uoto wa asili ndani ya hifadhi hiyo kwa kukata miti kwa ajili ya mbao bila kibali kutoka kwa mkurungezi wa wa wanyamapori.

Katika shauri hilo la jinai namba 223/2018 Washitakiwa wote wamekili kutenda kosa la kuingia hifadhi kinyume na kifungu namba 15 cha sheria ya uhifadhi wanyama pori namba 5 ya mwaka 2009.

Hata hivyo hoja za msingi zitasomwa Mahakamani hapo June 29 mwaka huu na watumiwa wote wamerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
Share:

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA YA KUMSABABISHIA UJAUZITO MWANAFUNZI


Na Lilian Katabaro
KAHAMA.

Mkazi wa kijiji cha Ufala Wilayani KAHAMA, JOSHUA ANDREW amefikishwa katika mahakama ya Wilaya hiyo kwa tuhuma ya kubaka na kumsababishia ujauzito mwanafunzi wa miaka 16 kinyume na sheria.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, USHINDI SWALLO, Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi, FELIX MBISE amesema ANDREW alitenda kosa May 31 mwaka huu saa 2 asubuhi katika kijiji cha Ufala ambapo alimbaka mwanafunzi huyo na kumsababishia ujauzito.

FELIX amesema katika shauri hilo la jinai namba 215/2018 ANDREW anatuhumiwa kwa kosa la kwanza la kubaka kinyume na kifungu 130 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Amesema kosa la pili, ANDREW anatuhumiwa kumsababishia mwanafunzi ujauzito kinyume na kifungu namba 60 A cha sheria ya elimu sura ya 353 kanuni ya adhabu ya mwaka 2016.

ANDREW amekana kutenda kosa hilo na upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na shauri hilo litatajwa tena mahakamani hapo June 23 mwaka huu na amerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
Share:

MBUNGE WA ZAMANI WA JIMBO LA KAHAMA JAMES LEMBELI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JUMATANO



KAHAMA.

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuanzia mwaka 2005 hadi 2015, JAMES LEMBELI, siku ya Jumatano atazungumza na Vyombo vya Habari nyumbani kwake kijijini Mseki Bulungwa wilayani Kahama.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Msaidizi wake, MIPAWA NG’WANANGOLELWA jana, katika mkutano huo LEMBELI ataelezea ushiriki wake katika ujenzi wa taifa na mustakabali wake katika masuala ya kisiasa.

NG'WANANGOLELWA amesema, LEMBELI ambaye katika kipindi chake cha ubunge alipata umaarufu katika mapambano dhidi ya ufisadi nchini, ameamua kuzungumza na vyombo vya habari baada ya ukimya wa muda mrefu.

Kabla ya kujiunga na siasa mwaka 2005, LEMBELI amewahi kufanya kazi katika taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na iliyokuwa Jumuiya ya WASHIRIKA, gazeti la Kiongozi, Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (DW) jijini Berlin na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Katika hatua nyingine, Waislamu nchini wameombwa kuwaombea viongozi wa Taifa la Tanzania bila kujali itikadi zao ili kuleta amani na kuwafanya viongozi wawe na Heshima na Busara katika kuongoza Watanzania na Taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa jana na Mkurugenzi wa Kahama Fm JAMES LEMBELI wakati wa futari aliyoiandaa kwaajili ya waumini wa msikiti wa kijiji cha Iboja kata ya Ukune Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.

Amesema, viongozi wa kiroho katika hali ya kawaida wapo karibu na Mungu hivyo, maombi yao yatafika kwa urahisi kwake mwenyezi Mungu ambaye atashusha neema ya hekima kwa viongozi wa taifa letu na hivyo amani ya nchi yetu kutamalaki.

Ameongeza kuwa kwa kuwa mfungo mtukufu wa Ramadhani ni utekelezaji wa nguzo tano za Uislamu ikiwa ni pamoja na kusali,basi viongozi na waumini kwa ujumla wana wajibu wa kuliombea Taifa letu lizidi kudumisha amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Kwa upande wake, Sheikh wa Msikiti wa Kijiji cha Iboja, ATHUMANI MOHAMED amemshukuru LEMBELI kwa moyo wa upendo na ukarimu na kuongeza kuwa LEMBELI kila mwaka amekuwa na utaratibu wa Kuwafuturisha Waislamu wasio na uwezo na kutoa wito kwa watu wengine wenye uwezo kuiga mfano wake.
Share:

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI


Na Paulina Juma
KAHAMA.

Mkazi wa kijiji cha Mwabomba Kitongoji cha Bukindwasali Wilayani KAHAMA, YOHANA MASANJA (19 amefikiswa katika mahakama ya wilaya hiyo kwa tuhuma ya kumuua LETICIA NDAKI, mkazi wa kijiji hicho cha Mwabomba kinyume na sheria.

Akisoma shitaka hilo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo USHINDI SWALLO, mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi, PETER MASAU amesema MASANJA alitenda kosa hilo May 30 mwaka huu saa 5 asubuhi huko Mwabomba Kitongoji cha Bukindwasali wilayani Kahama.

MASAU amesema MASANJA ametenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo 2002.

Katika shauri hilo la jinai namba 17/2018 MASANJA hakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo limeahirishwa hadi June 25 mwaka huu litakapotajwa mahakamani hapo na amerudishwa rumande kwa kuwa kesi hiyo haina dhamana.
Share:

KAHAMA FM KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MISITU WAPANDA MITI 300 SHULE YA MSINGI NYAHANGA A NA MBULU


Na Samwel Nyahongo
KAHAMA.

Ukosefu wa elimu juu ya umuhimu wa upandaji miti kwa ajili ya uhifadhi wa Mazingira miongoni mwa wakazi wa wilaya ya KAHAMA Mkoani SHINYANGA imekua ni changamoto na kusababisha baadhi ya maeneo wilayani humo kukabiliwa na hatari ya kuwa jangwa.

Hayo yamesemwa na Mmoja wa Wadau wa Maendeleo wilayani humo, Bibi ASHA MSANGI (NAKYOO), katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani uliofanyika katika Shule za Msingi Nyahanga “A” na Mbulu mjini Kahama.

SANJARI na kuhimiza elimu ya mazingira kwa Wananchi, MSANGI amesema vyombo vya dola havina budi kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha vitendo vyovyote vya uharibifu wa mazingira vinakomeshwa wilayani humo na katika taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo BERNADETHA MLWANGWA ameishukuru Kahama fm pamoja na wadau wote walioshiriki kwa kuiona shule hiyo kwani changamoto ya kukosekana kwa miti katika shule yake ni kubwa.

Amewahakikishia Wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa kampeni hiyo wakiwemo Wawakilishi wa Wakala wa Misitu nchini (TFS), Umoja wa Wapanda Miti Kahama na Chama Kikuu cha Ushirika Wilaya ya Kahama (KAKU), kwamba watahakikisha miti yote iliyopandwa inatunzwa na kukua.

Katika hatua nyingine MLWANGWA ameiomba mamlaka ya mji safi na usafi wa mazingira mjini Kahama (KUWASA) kuwapunguzia bei ya bili ya maji ili waweze kupata unafuu katika umwagiliaji wa miti hiyo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nyahanga MICHAEL MAGILE amewaomba wananchi kutunza mazingira na kuacha kuharibu miundombinu hali ambayo itapunguza magonjwa ikiwemo magonjwa ya mlipuko.

Jumla ya miti 300 inatarajiwa kupandwa katika shule hizo za Msingi za Nyahanga “A” na Mbulu katika maadhimisho hayo ya Siku ya Mazingira Duniani nchini ya kampeni hiyo yenye kauli mbiu isemayo: OTESHA MITI-KAHAMA YA KIJANI INAWEZEKANA.

Siku ya Mazingira Duniani huadhimishwa kila Juni Tano ya kila Mwaka ambapo kimataifa kauli mbiu yake inasema: TOKOMEZA UCHAFUZIWA MAZINGIRA UNAOSABABISHWA NA MIFUKO MICHAFU YA PLASTIKI.

Kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam ambapo kaulimbiu ya kitaifa ni MKAA UNA GHARAMA, TUMIA NISHATI MBADALA.
Share:

WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUINGIA PORI LA AKIBA LA KIGOSI MOYOWOSI KINYUME CHA SHERIA


Na Lilian Katabaro
KAHAMA.

Wakazi wa kijijini cha Kilimahewa wilayani Kahama EZEKIEL CHARLES (52) na REVOKATUS MAGANGA (36) wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya hiyo kwa tuhuma za kuingia katika Pori la Akiba la Moyowosi-Kigosi na kupatikana na mchanga wenye madini bila kibali.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo IMANI BATENZI, mwendesha mashitaka wa Idara ya wanyama pori CATHERINE ALOYCE amesema washitakiwa walitenda kosa hilo Mei 30 mwaka huu majira ya saa nne usiku kwa kuingia ndani ya hifadhi bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori.

CATHERINE amesema katika shitaka la pili washitakiwa hao pia walikamatwa wakiwa na mchanga unaosadikika kuwa na madini ya dhahabu viroba vinne kinyume na kifungu namba 20 cha sheria ya uhifadhi wanyama pori ya mwaka 2009.

Katika shauri hilo la jinai namba 206/2018 Washitakiwa wamekiri kuingia katika Pori hilo la Akiba Moyowosi-Kigosi kinyume na kifungu namba 15 cha sheria ya uhifadhi wa wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.

Kosa la pili ni kupatikana na mchanga unaodhaniwa unamadini ya dhahabu kinyume na kifungu namba 20 cha sheria ya uhifadhi wanyamapori ya mwaka 2009.

Kufuatia hatua ya Washitakiwa kukiri makosa hayo, hoja za msingi zitasomwa Mahakamani hapo June 14 mwaka huu na watuhumiwa wote wamerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
Share:

ZAIDI YA WANAUME 35,000 MKOA WA SHINYANGA WAFANYIWA TOHARA


Na Sebastian Mnakaya
KAHAMA.

Zaidi ya wanaume 35,000 katika mkoa wa SHINYANGA wamefanyiwa tohara katika vituo mbalimbali mkoani humo katika kipindi cha Octoba mwaka jana hadi mwezi Machi mwaka huu, huku ikitarajiwa kuwafanyia wanaume 64,000 ifikapo Septemba mwaka huu.

Akizungumza leo na KAHAMA FM mshauri wa huduma za tohara kwa wanaume kutoka shirika la INTRAHEALTH INTERNATIONAL mkoani Shinyanga, Dkt ENNOCENT MBUGI amesema zoezi hilo linawalenga watoto kuanzia umri wa miaka 10 na watu wazima.

Naye mtoa huduma za tohara kwa wanaume katika hospitali ya Halmashauri ya mji wa Kahama, LINDA KIDOLEZI amesema kumekuwa na muitikio mdogo miongongoni mwa wanaume wenye umri kuanzia miakaa 20 na kuendelea ikilinganishwa na wale wa chini ya umri huo.

Kwa upande wao baadhi ya Wanaume waliofanyiwa tohara katika Hospitali ya mji wa Kahama wamesema wanajisikia fahari na kujiamini baada ya zoezi hilo kwani wana uhakika wa kuepuka maambukizi ya magonjwa ya ngono ukiwemo UKIMWI kwa asilimia kubwa.

Serikali kwa kushirikiana na Shirika la INTRAHEALTH INTERNATIONAL mwaka 2010 ilianzisha kampeni hiyo ya tohara bure kwa wanaume kuanzia miaka kumi hadi miaka 60, lengo likiwa ni kuwaepusha na uwezekano wa kuambukizana magonjwa ya ngono, hususan UKIMWI.
Share:

WATU WANNE WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAUAWA NA POLISI


Na Salvatory Ntandu
KAHAMA.

Watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuawa katika majibizano ya risasi baina yao na askari polisi katika Makaburi ya Kitwana wilayani Kahama, huku silaha nne za kivita na bomu moja la kutupa kwa mkono vikipatikana katika tukio hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mjini Kahama Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, SIMON HAULE amesema tukio limetokea jana majira ya saa sita mchana baada ya watuhumiwa hao kutaka kuwakimbia polisi waliokuwa wanawashikilia.

Amesema watu hao walikamatwa na Jeshi la Polisi katika mikoa ya Tabora, Katavi, Shinyanga na Kigoma ambapo walitoa ushirikano kwa jeshi la Polisi na kuonesha Mahali ambapo huwa wanaficha silaha hizo katika eneo la Makaburi ya Kitwana.

Naye Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Shinyanga aliyeendesha msako huo, AMADIUS TESHA amewataka Majambazi popote walipo kusalimisha silaha zao na wasipofanya hivyo hawatasalimika.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kitwana wamelipongeza jeshi la Polisi kufanikisha msako huo ambao umewezesha kukamatwa kwa silaha hizo.

Silaha zilizokamatwa ni pamoja na bunduki aina ya AK47 yenye risasi 30, Shotgun 1, Bastola 2 zenye risasi na Bomu moja la kutupa kwa mkono.
Share:

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels