Kaimu
Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo (wa pili kushoto)
akitoa salamu za UNESCO wakati maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani
ambapo huadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Februari yaliyofanyika mjini
Dodoma na kuhudhuriwa na waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya
jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau wengine wa habari
nchini. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith
Mahenge, Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Mh. Juliana Shonza (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa
Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina
Musaroche (wa kwanza kushoto).
Mkuu
wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina
Musaroche akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kaimu Katibu Mtendaji wa
tume hiyo Dk. Moshi Kimizi (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika Mjini Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge akizungumza machache
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza wakati wa sherehe za maadhimisho ya
Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana
Shonza akiwasili katika hoteli ya Nashera mjini Dodoma kushiriki sherehe
za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani akiwa ameambatana na Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge (kulia) pamoja na Katibu
wa Mtandao wa Radio za Jamii nchini (TADIO), Marco Mipawa (kushoto).
Kutoka
kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge, Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana
Shonza, Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith
Shayo pamoja na Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco
(NATCOM), Christina Musaroche wakiwa meza kuu wakati wa sherehe za
maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani mjini Dodoma.
Mratibu
wa Mtandao wa Vyombo vya Habari na Jinsia Kusini mwa Afrika (GEMSAT) ,
Gladness Munuo akitoa mada kuhusu usawa wa jinsia katika kuripoti
michezo, changamoto na taratibu zake wakati wa sherehe za maadhimisho ya
Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.
Katibu
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena akisisitiza umuhimu
wa maudhui katika vipindi vya redio ambapo aliwaasa kutangaza masuala
yanayowahusu wanajamii katika maeneo yanayohusika badala ya kuwalisha
wasikilizaji taarifa ambazo ziko nje na mipaka wanayoishi.
Mtaalamu
wa Vyombo vya Habari na Mawasiliano, Mariagoreth Charles akiwasilisha
kanuni za uandishi wa habari za mtandaoni na mitandao ya kijamii kwa
waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara
na Visiwani pamoja na wadau wengine wa habari nchini walioshiriki kwenye
maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.
Mtangazaji
Mkongwe wa Habari za Michezo nchini, Abdallah Majura amesema pamoja na
kwamba waandishi wanatangaza vipindi vya michezo lakini maudhui
hayakidhi na kuvutia vile inavyostahili akitoa mfano hai wakati
akichangia kwa nini waandishi wengi hawaandiki habari za michezo. Majura
amesema yeye mwenyewe amewahi kupata tuzo mbili kwa ajili ya vipindi
vya michezo.
Pichani
juu na chini ni sehemu ya waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya
jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau wengine wa habari
nchini waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani
yaliyofanyika mjini Dodoma.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana
Shonza (wa tatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt.
Binilith Mahenge (kushoto) pamoja na Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
nchini, Faith Shayo (wa tano kulia) wakicheza wimbo maalum wa ngoma za
asili wa Kikundi cha Kaza Roho cha mjini Dodoma ulioongozwa na Msanii
Mwinamila wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani
yaliyofanyika mjini Dodoma.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana
Shonza na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari
wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja
na wadau wengine wa habari nchini wakati wa sherehe za maadhimisho ya
Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.