Ahukumiwa Miaka 30 Jela Kwa Kumbaka Mtoto Bubu

Mahakama  ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, imemhukumu Ramadhani Shaban (24), Mkazi wa Mtaa wa Majengo B, kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 15, bubu ambaye pia ana upungufu wa akili.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Gosper Luoga, baada ya mshtakiwa kukiri kosa.

Awali, Mwendesha Mashtaka wa Serikali wa Mkoa wa Katavi, Flaviana Shio, alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 9, mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika Mtaa wa Majengo B.

Alidai kuwa siku ya tukio mshtakiwa alikwenda maeneo ya Mtaa wa Mjimwema alikokuwa akiishi mtoto huyo na mjomba wake, Ernest Chambala na kumpakia kwenye baiskeli yake.

Alisema alikwenda naye hadi kwenye chumba chake alichokuwa amepanga na kumbaka.

Aliendelea kuiambia mahakama kuwa baada ya tukio hilo mtoto huyo alitoka nje na kuanza kuwaonyesha watu kwa ishara kuwa amebakwa.

Mjomba wa mtoto huyo alianza jitihada za kumsaka mbakaji huyo kwa kumchukua mpwa wake huyo ambaye alimwongoza hadi kwenye nyumba alikofanyiwa unyama huo.

Alieleza kuwa majirani wa nyumba hiyo walipoulizwa kama walimuona mtoto huyo akiingizwa kwenye chumba cha mshtakiwa walikiri kumuona.

Baada ya kukamatwa alichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi na katika maelezo yake alikiri kutenda kosa hilo na taarifa za daktari zilithibitisha kuwa mtoto huyo alikuwa ameingiliwa na mwanaume kwa kuwa sehemu zake za siri zilikuwa na mbegu za kiume.

Mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo kwa kile alichodai amekuwa akifanya naye mapenzi mara kwa mara kwa sababu ni mpenzi wake.

Katika utetezi wake, mshtakiwa aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa mama yake mzazi anamtegemea na baba yake alishafariki.

Hakimu Luoga baada ya kusikiliza utetezi huo aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa amepatikana na hatia imemhukumu kwenda kutumikia jela miaka 30.

Alisema katika hukumu hiyo mahakama pia imezingatia ongezeko la matukio ya ubakaji wilayani humo.
Share:

Mwanafunzi Darasa la Tatu Apewa Mimba.....Serikali Yaagiza Wazazi Wake Wakamatwe

Serikali wilayani Nkasi mkoani Rukwa, imeagiza kukamatwa kwa wazazi wa mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Mkinga aliyepata ujauzito kwa kosa la kuandaa mpango wa kumuoza mwanafunzi huyo.

Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mtanda, wakati akikabidhi pikipiki 28 zenye thamani ya Sh. milioni 98 zilizotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, kwa kushirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Fedha hizo zilitolewa kwa ajili ya mpango wa kukuza stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu kwa waratibu kata wa wilaya hiyo.

Alisema katika kijiji cha Mkinga kuna mwanafunzi wa darasa la tatu amepata ujauzito na wazazi wake walikuwa wanaandaa mkakati wa kumuozesha, lakini walishindwa baada ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kuingilia kati na kuvuruga mpango huo.

"Naagiza wazazi wote wa mwanafunzi huyo wakamatwe mara moja, mwanafunzi huyo pamoja na aliyempa mimba wafikishwe katika vyombo vya dola, ili sheria ichukue mkondo wake na ninyi waratibu elimu kata tambueni mna jukumu kubwa la kuhakikisha mimba hizi zinakwisha, " alisema.

Mtanda alisema hali hiyo inaonyesha kuwa bado tatizo la mimba ni kubwa kwa sababu katika mwezi uliopita jumla ya wanafunzi 27 walipata ujauzito, hivyo bado kuna kazi kubwa ya kufanya.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Misana Kwangula, alisema lengo la serikali kuwapatia pikipiki hizo ni kuwawezesha kutembelea shule zilizopo katika kata zao kwa kuwa walikuwa wanalalamika kuwa hawana vitendea kazi vya kuwawezesha kufanya ukaguzi katika shule wanazozisimamia.
Share:

Mwanafunzi auawa kwa kisu kwenye kigodoro akigombea mwanamke

 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikiliwa mwanafunzi anayetuhumiwa kumuua mwenzake mwenye umri wa miaka kumi na tisa wote wakiwa wanasoma Shule ya Sekondari Mteule akituhumiwa kumchoma kisu sehemu kifuani wakiwa kwenye kigodoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa amemtaja aliyeuawa ni Abdulrahiman Daud aliyeshambuliwa kwa kile kinachodaiwa ugomvi wa kugombea mwanamke.
 
==>>Msikilize Kamanda Mutafungwa akiongea hapo chini.. BOFYA HAPA
Share:

Ashitakiwa Kwa Kujiita Mtoto wa CAG na Kisha Kubaka

Mkazi wa Mwananyamala, Ahmed Mudhihiri (26), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni,   Dar es salaam akikabiliwa na mashtaka matatu yakiwamo ya ubakaji na kufanya udanganyifu kuwa yeye ni mtoto wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Caroline Kiliwa, Mwendesha Mashtaka, Neema Moshi, alidai Julai 6  katika eneo la Hoteli ya White Sands  Mbezi Africana   Dar es Salaam, mshitakiwa alimbaka binti (jina limehifadhiwa).

Shitaka la pili ni kuwa  kati ya Juni 17 na Julai 7 mwaka huu   Dar es Salaam, alidanganya kuwa yeye ni Mwamvita Makamba.

Katika shitaka la tatu, mshitakiwa alidaiwa kati ya Juni 18 na Julai 7 mwaka huu, Dar es Salaam, alijitambulisha kuwa yeye ni Edd mtoto wa   CAG.
Share:

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Yasema ni kosa la jinai kudhihaki au kukejeli noti na sarafu za Tanzania.


Benki Kuu ya Tanzania imewataka wananchi kuheshimu fedha ya Tanzania kwani ni moja ya alama ya taifa.
Kauli hiyo imekuja kufuatia matukio ya hivi karibuni ya baadhi ya wananchi kutoziheshimu, kuzifanyia dhihaka na kebehi noti za Jamhuri ya Mungano wa Tanzania.
 
Taarifa ya BoT kwa vyombo vya habarI ambayo inasema utunzaji mzuri wa fedha zetu utapunguza uwezekano wa fedha hizo kuchakaa mapema na kupunguza gharama za uchapishaji.
"Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006, kifungu cha 26, BoT ndiyo taasisi pekee yenye mamlaka ya kutoa noti na sarafu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," imesema taarifa hiyo.

Pia imesema noti na sarafu hizo zina alama muhimu inayolitambulisha taifa la Tanzania ambayo ni nembo ya Bwana na Bibi. Imefafanua alama hiyo inapaswa kuheshimwa kama zilivyo alama nyingine kwa mfano Bendera ya Taifa.

Pia noti na sarafu zote zimetengenezwa kutoa thamani ya kisheria (legal tender) kama ilivyoandikwa juu ya noti au sarafu husika na pia Benki Kuu pekee ndiyo yenye mamlaka ya kuharibu noti na sarafu.

Taarifa hiyo imefafanua kuhusu hilo kupitia kifungu cha  28 kikisomwa pamoja na kifungu cha 30 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.

"Benki Kuu inatoa rai kwa wananchi kuzitunza fedha zetu kwa kuwa ni mojawapo ya tunu na alama muhimu ya uchumi wa nchi yetu.

"Vilevile, utunzaji mzuri wa fedha zetu utapunguza uwezekano wa fedha hizo kuchakaa mapema na kupunguza gharama za uchapishaji," imesema taarifa hiyo ya BoT.
Share:

Waziri Jafo Awataka Maofisa Elimu Kuacha Kuwanyanyasa Walimu

Waziri  wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amewaagiza maofi sa wa elimu wa mikoa na wilaya kuzingatia maadili kwa kuepuka vitendo vya upendeleo na unyanyasaji wa walimu na wanafunzi.

Pia amewataka kujiepusha na suala la uvujishaji mitihani, rushwa na utovu wa maadili. Katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Waziri Joseph Kakunda wakati wa kufungua kikao kazi cha siku mbili kilichowakutanisha maofisa elimu wa mikoa na halmashauri kilichofanyika jijini hapa, Jafo alihimiza umuhimu wa kuzingatia maadili na kusisitiza kuwa siku za hivi karibuni, sekta hiyo imejijengea picha mbaya kwa mambo kadhaa.

“Tunatakiwa kuepuka vitendo vya upendeleo na unyanyasaji wa aina yoyote kwa walimu na wanafunzi, uvujaji wa mitihani, rushwa na utovu wa maadili kwa sababu ninyi ni kioo cha jamii,” alisema. 
Jafo alionya kuwa vitendo vya utovu wa maadili kamwe havitavumiliwa na serikali na yeyote anayeendekeza vitendo hivyo atachukuliwa hatua kali.

“Nitumie fursa hii kulaani vitendo vya unyanyasaji na ukatili vilivyofanywa na baadhi walimu katika Shule ya Msingi Kibeta.”
 Aidha, Jafo aliwaasa viongozi hao kusimamia sheria, kanuni na taratibu katika utoaji wa adhabu kwa wanafunzi kote nchini. 
Alitumia nafasi hiyo kutoa msisitizo kwa viongozi hao kuwajibika kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na kuitumikia umma, watumishi, wadau na marafiki wa elimu ili kuendeleza imani iliyojengwa kwa umma.

Mkutano huo umewakutanisha watendaji wa elimu katika ngazi ya taifa, mikoa na halmashauri kwa lengo la kukumbushana majukumu, kujipima na kujitafakari utendaji, kupeana uzoefu, kujenga uwezo na kujadiliana juu ya mbinu na mikakati itakayotumika kusaidia kuboresha utoaji wa elimu bora.
Share:

Waziri Mkuu: Matumizi Ya Dawa Za Kulevya Yapungua Kwa 90%


WAZIRI MKUUKassim Majaliwa amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yamepungua kwa asilimia 90 baada ya Serikali kufanikiwa kudhibiti biashara hiyo.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Septemba 17, 2018) baada ya kufungua mkutano wa 28 wa wakuu wa vyombo vinavyopambana na dawa za kulevya kutoka nchi za Afrika ujulikanao kama (28th HONLEA- Afrika), jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNICC), unashirikisha wajumbe zaidi ya 120 kutoka nchi 54 za Afrika unatarajiwa kutoka na maazimio ya namna ya kutokomeza biashara ya dawa za kulevya katika mataifa hizo.

Waziri Mkuu amesema lengo la mkutano huo ni kubadilishana uzoefu na kupanga mikakati ya pamoja kuhusu udhibiti na mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya katika nchi hizo.

“Ni lazima tuwe na mikakati ya pamoja ya kudhibiti uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya barani Afrika. Hata hivyo ni muhimu kudhibiti njia zote zinazotumika kusafirisha dawa za kulevya.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Tanzania inaendelea na mikakati ya kupambana na uzalishaji wa dawa hizo ikiwemo mirungi na bangi, ambayo inapandwa kwa kuchanganywa na mazao ya chakula.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Tanzania ni nchi ya kwanza katika bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuanzisha vituo vya utoaji wa matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya mwaka 2011.

Amesema hadi kufikia mwishoni mwa 2017, jumla vituo sita vya kutolea matibabu vilianzishwa, ambapo zaidi ya waathirika 6,500 wa dawa za kulevya aina ya heroin walijiandikisha na kupatiwa matibabu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yameathiri sekta mbalimbali ikiwemo ya afya, uchumi na jamii, uchunguzi umebainisha kuwa kati ya asimilia 20 hadi 50 ya watumiaji wanamaambuzi ya ugonjwa wa ukimwi.

Amesema ni muhimu kwa nchi zote kuunga mkono na kuimarisha mifumo ya kisheria ya kimataifa katika udhibiti wa biashara za dawa za kulevya, ambao hutegemea mikataba yote ya msingi ya Umoja wa Mataifa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU.
Share:

Kamati ya Kusimamia Ngumi za Kulipwa Tanzania yatoa ufafanuzi kuhusu suala la Hassan Mwakinyo

UFAFANUZI KUHUSU SUALA LA HASSAN MWAKINYO
Kama mnavyokumbuka, majuma mawili yaliyopita nchi yetu ilipata sifa kubwa sana kwenye tasnia ya michezo hususan mchezo wa ngumi za kulipwa baada ya Hassan Mwakinyo kumpiga Sam Eggington kwa TKO raundi ya pili katika pambano la raundi 10 lisilo la mkanda lililofanyika tarehe 8 Septemba, 2018 huko Birmingham, Uingereza. Ushindi wa Mwakinyo, uliipeperusha vyema bendera ya nchi yetu.

Aliporejea kutoka Uingereza, Mwakinyo alipata mwaliko wa kufika katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya ijumaa tarehe 14 Septemba, 2018. Pamoja na kumpa pongezi, wabunge walimpatia zawadi kwa kulitangaza vyema taifa letu.

Mara baada ya kutoka bungeni, akiwa katika viwanja vya bunge, Mwakinyo alifanya mkutano na waandishi wa habari, pamoja na mambo mengine, alizungumzia safari yake ilivyokuwa mpaka amefanikiwa kupata ushindi. Mwakinyo aliueleza umma kwamba alipata changamoto nyingi kwenye safari hiyo kama vile kulazimika kukopa hela ya viza kutoka kwa mwanafunzi na kusafiri bila ya kibali na hivyo kulazimika kusafiri kama mkimbizi.

Kamati inapenda kutolea ufafanuzi suala la kibali na kwa uchache kuhusu suala la viza. Kwanza si kweli kwamba Mwakinyo amesafiri bila ya kupata kibali, wakala aliyekwenda na Mwakinyo aliwasilisha maombi yake ya safari hiyo ndani ya siku 7 kabla ya safari. Kamati iliyajadili na kupitia kumbukumbu mbalimbali za Mwakinyo pamoja na mpinzani wake na iliridhia kumwombea kibali ili aweze kusafiri kwa ajili ya pambano hilo. Maombi ya kibali toka katika Kamati kwenda katika Baraza la Michezo la Taifa (BMT) yaliwasilishwa tarehe 3 Septemba, 2018 kwa “maombi ya dharura” na tarehe 5 Septemba, 2018 Kibali kilitolewa na nakala yake kutumiwa wakala aliyewasilisha maombi hayo ndugu Rashid Nassor ambaye ndiye aliyesafiri naye siku hiyo hiyo.

Ndugu waandishi wa habari, naomba ikumbukwe kwamba, kwa mujibu wa Kanuni za BMT, maombi ya vibali vya kusafiri nje ya nchi kwa shughuli za kimichezo yanapaswa kuwasilishwa siku 14 kabla ya safari. Inapoonekana kwamba safari hiyo ina tija kwa mchezaji na taifa kwa ujumla, BMT hutumia busara na kutoa kibali nje ya muda kama ilivyofanya kwa Mwakinyo ambaye alipata kibali ndani ya siku 2 tu. Hivyo, napenda kusisitiza kwamba, Hassan Mwakinyo alipata kibali kama nilivyoeleza hapo juu na nichukue fursa hii kumwomba radhi Katibu wa BMT pamoja na watendaji wote kwa kadhia hii.

Vilevile, kwa kifupi, napenda ifahamike kwamba, suala la viza ni jukumu la promota na wakala/bondia mwenyewe na pesa hiyo huwa inarudishwa na promota wanapofika huko kwenye pambano. Hivyo, tunasikitika kwa changamoto hiyo aliyopitia kupata visa lakini tunaamini kuwa wamerudishiwa na labda wakala aliyekwenda naye ndugu Rashid Nassor anaweza kulitolea ufafanuzi zaidi.

Mwisho, Kamati inapenda kuchukua fursa hii kumpongeza tena Hassan Mwakinyo kwa ushindi wake na iko tayari kumshauri kuhusu mustakbali wake mara baada ya ushindi huo kama ataona inafaa.

Imetolewa na:
Yahya Poli
Katibu – Kamati ya Kusimamia Ngumi za Kulipwa Tanzania.
17 Septemba, 2018
Share:

Ahukumiwa kwenda Jela Miaka 6 Kwa Kumkashifu Rais Magufuli


Yuston Emanuel (31) mkazi wa Ngara mkoani Kagera amehukumiwa kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya Sh200, 000 kwa kosa la kutumia lugha ya dhihaka dhidi ya Rais John Magufuli.

Hukumu hiyo ilitolewa leo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi  Septemba 17, 2018 wilaya ya Misungwi, Erick Marley baada ya kuridhika bila shaka yoyote na ushahidi wa upande wa Jamhuri kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Katika shauri hilo la jinai namba 27/2018, upande wa Jamhuri ulioongozwa na mwendesha mashitaka wa polisi, Ramsoney Salehe uliita mashahidi watano kuthibitisha kosa.

Akisoma maelezo ya kosa, mwendesha mashitaka huyo aliiambia Mahakama mshtakiwa alitenda kosa hilo saa 10:00 jioni ya Juni 25 akiwa eneo la kivuko cha Kigongo wilayani Misungwi.

Alidai akiwa eneo hilo, mshtakiwa aliyekuwa akivuka kutoka Kigongo wilayani Misungwi kwenda Busisi wilayani Sengerema alitumia maneno ya dhihaka dhidi ya Rais John Magufuli kwa kutamka "Rais Magufuli kitu gani bwana"

Salehe aliiambia mahakama kosa hilo ni kinyume cha kifungu cha 89 (1) (a) kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

“Naiomba Mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wanaotoa lugha ya kumdhihaki Rais Magufuli kama alivyofanya mshtakiwa ambaye Rais (Rais John Magufuli) anaweza kuwa mzazi wake,” alisema Salehe.

 Akijitetea baada ya kutiwa hatiani, mshtakiwa aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu na kumsamehe kwa sababu ni kosa lake la kwanza.

Mpaka muda wa Mahakama unamalizika jana, mshtakiwa alishindwa kulipa faini na hivyo kupelekwa gereza kuanza kutumikia kifungo cha miezi sita jela.
Share:

Makonda Alipongeza Jeshi la Polisi kwa Kusimamia Amani Uchaguzi Ukonga

 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa ya kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kipindi chote cha kampeni za uchaguzi Jimbo la Ukonga hadi uchaguzi uliofanyika siku ya Jana na kumalizika salama pasipo uvunjifu wa amani.

RC Makonda ametoa pongezi hizo leo alipokutana na Makamanda na maafisa wa polisi ambapo amesema anajivunia kuona uchaguzi wa Ukonga umemalizika salama bila fujo wala uvunjifu wa amani.

Aidha RC Makonda amewapongeza wananchi kwa kulinda aman na kulifanya jiji la Dar es salaam kuzidi kuwa na amani masaa 24.

Pamoja na hayo RC Makonda amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na Kamanda wa Polis Kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa kwa kuwa na vijana shupavu, wakakamavu na wenye morali ya kuwatumikia wananchi.
Share:

Waziri Mkuu: Ulaji Usiofaa Unaongeza Magonjwa Yasiyoambukiza

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesemalishe duni pamoja na ulaji usiofaa na mitindo ya maisha vinachangia kwa kiasi kikubwa katika ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza hususan kwa vijana na watu wazima, ambao ndiyo nguvu kazi kwa Taifa.

“Ni jambo lisilopingika kuwa hatua za kukabiliana na magonjwa ya kusendeka (mfano matatizo ya moyo, saratani, kisukari na shinikizo kubwa la damu) zinachangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza kasi ya maendeleo yetu kwani gharama za matibabu yake ni kubwa mno; si kwa kaya zinazoathirika tu bali kwa Taifa zima.”

Waziri Mkuu  ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Septemba 11, 2018),  wakati akifungua mkutano wa tano wa wadau wa masuala ya lishe, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kambarage, Hazina jijini Dodoma. 

Waziri Mkuu amesema lishe iliyozidi inadhihirishwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukizwa yanayotokana na mabadiliko ya mitindo ya maisha na ulaji usiofaa kama vile uzito uliozidi, viriba tumbo, shinikizo la damu pamoja na kisukari.

Amesema kasi ya ongezeko la magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza inapaswa kudhibitiwa kwa kuzingatia ulaji unaofaa na mtindo bora wa maisha. “Huu ni wakati wa kuangalia kwa pamoja kama jitihada zetu zinaleta matunda tunayotarajia.”

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua kuwa lishe bora ni msingi wa maendeleo ya Taifa letu hivyo, uwepo wao katika mkutano huo unaonesha umuhimu wa kuimarisha ushiriki wa kila sekta, kila mdau ikiwemo sekta binafsi kwa nafasi yake katika kupambana na aina zote za utapiamlo. 

Amesema ushiriki wa kila sekta ni wa muhimu kwa sababu hakuna sekta moja pekee inayoweza kuondoa tatizo la utapiamlo, pia ni vema kwa wadau hao wakajitathmini mmoja mmoja katika sekta zao kuona kama wanaelekea katika muelekeo sawa na mipango ya Serikali.

“Kwa kuzingatia hilo, ofisi yangu imeweka utaratibu maalum wa kuratibu utekelezaji wa kazi za lishe nchini, ambapo kamati ya Kitaifa ya Usimamizi na Ushauri kuhusu masula ya lishe nchini yaani High Level Steering Committee on Nutrition imeundwa ili kusimamia utekelezaji wa azma hiyo.” 

Waziri Mkuu amesema kwamba watu wote wanatambua jitihada kubwa zilizowekwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau katika kupambana na matatizo ya lishe nchini, ambapo taarifa za wataalamu zinasema kuwa kwa sasa nchi inakabiliwa na aina mbili za utapiamlo yaani lishe duni na lishe iliyozidi au iliyokithiri. 

Amesema walengwa wakubwa wa lishe duni ni pamoja na watoto chini ya miaka mitano, wanawake walio katika umri wa kuzaa hususani wajawazito na wanaonyonyesha pamoja na vijana balehe (hususan wa kike). “Hii ni kwa sababu mahitaji ya virutubishi kwa ajili ya miili yao ni makubwa, ukilinganisha na ule unaohitajika na makundi mengine.” 

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU.
Share:

Muhimbili Yatumia Mil 600 Kwa Mwezi Kuhudumia Wasiojiweza

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), inatumia kati ya Sh. milioni 450 hadi Sh. milioni 600 kila mwezi kugharamia wagonjwa wanaoshindwa kulipia matibabu yao.

Hayo yalielezwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru alipokuwa akimkabidhi msaada wa baiskeli ya matairi matatu, Said Mtonga ambaye amekatwa miguu yote miwili kutokana na maradhi yanayomsumbua.

“Jukumu letu ni kutibu lakini inapobidi huwa tunaenda zaidi ya hapo na kutoa msaada ‘rehabilitation’, kwa mgonjwa kama huyu, ili anapotoka hapa aweze kwenda kuendelea na majukumu yake, ajenge uchumi wa nchi na wake pia.

“Hivyo, hospitali imegharamia matibabu yake yote kwa kuwa hakuwa na uwezo wa kulipia na kwa mwezi huwa tunatumia kiasi cha kati ya Sh. milioni 450 hadi Sh. milioni 600,” alisema.

Ofisa Ustawi wa Jamii Muhimbili, Wodi ya Kibasila, John Mwakyusa alisema matibabu ya Said yamegharimu Sh. 935,000 tangu alipofika hospitalini hapo Mei, mwaka huu. .

“Alikukuja miguu yake ikiwa imevimba na ina vidonda, alichunguzwa na kuonekana haikuwa saratani, madaktari wakamfanyia upasuaji kukata mguu wake mmoja lakini baadae mguu uliobaki nao ulionyesha tatizo, nao ukakatwa.

“Ndugu zake hawakuwahi kujitokeza, tukawatafuta lakini tulipowapata walitueleza hawakuwa na uwezo wa kumsaidia, hata marafiki zake pia hawakuja,” alisema.

Alisema waliendelea kumtibia hadi alipopona kabisa wakaona ni vema kumtafutia baiskeli ili aweze kutembelea.

“Tunamshuruku mkurugenzi alitupatia Sh. 500,000 tukaenda SIDO kutafuta Sh. 80,000 tukampa mtaji,” alisema.

Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii Muhimbili, Emmanuel Mwasota alisema ugonjwa uliokuwa ukimsumbua Said kitaalam unaitwa Septic Wound with Gangrene.

Share:

Mbunge CUF Apigilia Msumari Sakata la Makontena ya Makonda

Mbunge wa Konde, Khatibu Saidi Haji (CUF), amemsifu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kwa ‘kuyang’ang’ania’ makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akimtaka kuyalipia kodi.

Makontena hayo ambayo yaliingizwa Bandari ya Dar es Salaam kwa jina la mkuu huyo wa mkoa yakidaiwa kuwa na samani za walimu wa shule mbalimbali za Mkoa wa Dar es Salaam ambapo yalitakiwa kulipiwa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), yakitakiwa kulipiwa kodi suala lilioungwa mkono na Waziri Mpango na kuamuru yazuiliwe hadi yatakapolipiwa kodi na yasipolipiwa yapigwe mnada huku Rais John Magufuli akipigilia msumari wa mwisho kumtaka Makonda ayalipie kodi makontena hayo.

Akichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia Baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), bungeni jijini Dodoma leo Jumatano Septemba 11, Haji amesema mawaziri wa aina ya Dk. Mpango ndiyo Rais Magufuli anaowataka.

“Mheshimiwa sheria ni msumeno na katika kutekeleza majukumu yako muhimu ya kusimamia fedha za nchi hii hutakiwi kumwangalia usoni yeyote anayevunja sheria za nchi hii katika kusimamia kodi za wananchi.

“Kwa hiyo kitendo chako kitabakia katika historia, alijaribu kuwachezea wengine lakini alichezea vyeupe amekutana na cheusi kimemtia doa, na nakuambia Dk. Mpangio uzi ni huo huo mbane Makonda hadi mwisho ili haki ipatikane,” amesema Khatibu.
Share:

Uteuzi Uliofanywa na Rais Magufuli Muda Mfupi Kabla ya Kuwaapisha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania John Pombe Magufuli amefanya uteuzi mwingine na kumteua Balozi Dkt.  Aziz Ponary Mlima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda.

Kufuatia uteuzi huo Balozi Mlima anatarajia kuapishwa leo Septemba 12, 2018 Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma.

Pia Septemba 3, 2018 Rais Magufuli alifanya uteuzi wa Dkt. John Antony Kiang’u Jingu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambapo kabla ya uteuzi huo Kingu alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye naye atakula kiapo leo.

Aidha, naye Kamishna wa Polisi Diwani Athumani aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU anatarajia kuapishwa leo Chamwino Jijini Dodoma.
Share:

Benki Zinazotoa Mikopo Ya Kilimo Tanzania Bara Na Zanzibar Zatakiwa Kufuata Vigezo Vya Ukopeshaji

Serikali imezitaka Benki zote zinazotoa mikopo ya kilimo Tanzania Bara na Zanzibar kuhakikisha zinatoa mikopo kwa kuzingatia vigezo vya ukopeshaji vikiwemo kuangalia historia ya mkopaji ili kuondoa mikopo Chechefu (NPL).

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Bububu Mhe. Mwantakaje Haji Juma, aliyetaka kujua utaratibu unaotumika kutoa mikopo kwa wakulima wa Zanzibar kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).

Dkt. Kijaji alieleza kuwa kabla ya kutoa mkopo ni lazima Benki ijiridhishe na aina ya mradi wa mkopaji ikiwa utaleta faida itakayomuwezesha mkopaji kurejesha mkopo huo kwa wakati ili kuzuia ukuaji wa Mikopo Chechefu.

Akijibu swali la msingi la Mbunge huyo aliyetaka kujua ni wananchi wangapi wanaonufaika na mikopo ya Kilimo kwa upande wa Zanzibar, Dkt. Kijaji alisema kuwa jumla ya wananchi 3,000 wamenufaika na mikopo ya Benki ya TADB hadi kufikia Julai 31, 2018.

“Kati ya wanufaika hao 3000, idadi ya wanaume walionufaika ni 1800, wanawake 900 na vijana wa kike na kiume ni 300”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa jumla ya mikopo ya shillingi bilioni 6.50, imetolewa kwa wananchi hao wa Zanzibar hadi kufikia Julai 31, 2018.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango.
Share:

Mahakama ya uhalifu ya kivita ICC kuwekewa vikwazo na Marekani endapo itaendelea kuwashtaki raia wake

Marekani imetishia vikwazo dhidi ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC ikiwa itaendelea na mikakati yake ya kuwashtaki raia wa Marekani.Mahakama hiyo kwa sasa inatathmini kuwafungulia mashtaka wanajeshi wa Marekani kwa madai ya kuwatesa wafungwa nchini Afghanistan.

Mshauri wa masuala ya usalama ya kitaifa John Bolton alisema mahakama hiyo sio halali na kuapa kuwa Marekani itafanya kila iwezalo kuwalinda raia wake.

Baada ya tamko hilo kutoka marekani ikumbukwe kuwa wakati fulani mwaka uliopita nchi tatu za Afrika – Burundi, Gambia na Afrika Kusini ziliashiria nia yao ya kujitoa kutoka mahakama hiyo ya kimatafa ya uhalifu wa kivita ICC. Kulikuwa na hofu kuwa nchi zaidi zingefuata.

Mwezi Oktoba mwaka 2016, Burundi na Afrika Kusini waliandika kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuelezea uamuzi wao wa kuondoka kutoka ICC.

Wakati huo, nchi ya Gambia ambayo ni nchi ndogo ambayo sehemu yake kubw iko ndani ya Senegal magharibi mwa Afrika ilitangaza kuwa ingejitoa. Lakini hatua hiyo ilifutwa mara wakati serikali mpya iliingia madarakani.

Tangu wakati huo hatua hatua za nchi za Afrika kujitoa kutoka ICC huzijafua dafu, hata baada ta Muunganoa wa Afrika kutoa kauli ya pamoja na kujitoa kutoka mahaka hiyo.

“Kundi la watu wasio na maaana,” rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati mmoja aliielezea ICC, huku rais wa Rwanda Paul Kagame akisema kuwa mahakama haikuwa kwa minajili ya haki bali siasa zinazotajwa kuwa haki ya kimataifa.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye wakati mmoja alikabiliwa na kesi katika mahakama hiyo alisrma makahama hiyo ni chombo ya siasa za dunia lakina sio kuhusu haki ilizotakiwa kuteleleza.

Kurodhika na mahakama hiyo kumetokana na hisia kuwa ICC ilikuwa inawalenga waafrika na haieshimu siasa na uhuru wa nchi za Afrika. Keshi kumi kati ya tisa zilizo, kwenye mahakama hiyo zinahusu nchi za Afrika.

Mahakama hiyoi inachunguza na kuwaleta hukumuni wale wanaohusika kwenye uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, ikiingilia kati wakati mahakama za nchi haziwezi kuwahukumu.

ICC ilibuniwa chini ya mkataba wa Roma wa mwaka 2002 na imeungwa mkono na nchi 123 ikiwemo Uingereza.

Baadhi ya nchi za Afrika zimataja kuondoka kutoka mahakam hiyo zikisema kuwa inazionea nchi za Afrika.
Share:

Kamishna Wa TRA Apata Ajali Dodoma

Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere amepata ajali leo Jumanne, Septemba 11, 2018 baada ya gari lake aina ya Toyota Land Cruiser V8 namba STL 5199 kugongana na gari dogo la mtu binafsi lenye namba za usajili T 416 BTH, eneo la Nanenane, jijini Dodoma.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema, ajali hiyo imetokea na kwamba hakuna madhara kwa binadamu bali ni uharibifu wa magari ndio umetokea.

Gari la Mamlaka ya Mapato lilikuwa likitokea Morogoro kuelekea Dodoma ndipo lilipogongana na gari lililokuwa likielekea chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambalo lilichomoza wakati gari la Kamishna likipita gari jingine.

Amesema gari la Kamishna lilikuwa likiendeshwa na Peter (35) kabila ni Msukuma ambaye ni mkazi wa Kurasini Dar es salaam huku lile jingine lilikuwa linaendeshwa na Paul (39) kabila ni Masai ambaye ni mhadhili wa Chuo Kikuu cha UDOM.

Ameweka wazi kuwa wamejiridhisha mpaka sasa kiafya wahusika wote wako salama.
Share:

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA WIZI

Image result for MAHAKAMANI NYUNDO
Na Lilian Katabaro
KAHAMA.

Mkazi wa mtaa wa Nyasubi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga DENICE KIZENGA (21) amefikishwa mbele ya Mahakama ya Wilaya hiyo kwa tuhuma ya wizi wa kuaminika kinyume cha sheria.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo USHINDI SWALO mwendesha mashitaka wa Polisi SAADA ADAM amesema KIZENGA alitenda kosa hili Septemba 4 mwaka huu majira ya saa 2 asubuhi huko mtaa wa majengo aliiba belo mbili za vitenge zenye thamani ya shilingi 3,800,000 mali ya DAUD RICHARD.

SAADA amesma KIZENGA ametenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 273 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002.

Katika shauri hilo la jinai namba 32/2018 KIZENGA amekana kutenda kosa hilo na upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na mshitakiwa amerudishwa rumande kwa kukosa dhamana na shauri hilo kutajwa tena Mahakamani hapo Septemba 25 mwaka huu.
Share:

HALMASHAURI YA MSALALA - KAHAMA YATENGA MIL. 15 ZA PIKIPIKI ZA MAAFISA UGANI KURAHISISHA UTENDAJI

Image result for pikipiki mpya
Na Salvatory Ntandu
KAHAMA

Halmashauri ya MSALALA Wilayani KAHAMA Mkoani SHINYANGA imetenga shilingi milioni 40 ili kununua pikipiki 15 za Maafisa Ugani ili kurahisisha utendaji kazi.

Kauli hiyo imetolewa jana Afisa kilimo wa Halmashauri ya Msalala ZEDEKIA SOLOMONI wakati akiwasisha Mada kwenye Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa Shirika lisilo la kiserikali la CABUIPA kwa kushirikiana na shirika la OXFAM iliyofanyika Mjini Kahama.

Amesema katika mwaka wa fedha wa 2018/19 Wametenga fedha hizo ili kutekeleza agizo la Serikali la kuwapatia Maafisa ugani Usafiri ili kutoa huduma bora za kilimo kwa wakulima katika maeneo yao.

Katika Hatua nyingine ZEDEKIA amewataka Wakulima kuzingatia Maelekezo ya Serikali juu ya Mabadiliko ya Tabia nchi kwa kupanda Mazao yanayostahimili ukame na kuachana na kilimo cha Mazoea.
Mradi wa kupunguza athari za maafa na majanga unatekelezwa na shirika la CABUIPA kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Uingereza (OXFAM) katika Halmashauri hiyo kwa miaka miwili kwa lengo la kupunguza ukame kwa kuwapatia wananchi elimu juu ya mabadiliko ya tabia nchi.
Share:

VIONGOZI WA SUNGUSUNGU KATA YA NYANDEKWA KAHAMA WAPIGA MARUFUKU MIFUGO KUSAFIRI USIKU

Image result for PICHA ZA ASKARI WA SUNGUSUNGU
Na William Bundala
KAHAMA.

Uongozi wa Sungusungu katika kata ya NYANDEKWA Wilayani KAHAMA Mkoani SHINYANGA umepiga marufuku watu wanaosafirisha mifugo usiku kupita katika eneo hilo,ikiwa ni pamoja na madereva boda boda wanaosomba watu na mizigo usiku kutofanya shughuli hizo.

Wito huo umetolewa na Mtemi wa Kata wa Sungusungu katika kata hiyo KABHILO MACHIBYA katika mkutano wa kata wa sungusungu uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Nyandekwa.

MACHIBYA Amesema kumekuwa na wizi mkubwa wa mifugo na mazao katika kata hiyo hali inayohatarisha amani na usalama na kwamba mtu yoyoye atakayepitisha mifugo usiku akamatwe na kuweka chini ya ulinzi yeye pamoja na mifugo yake.

Katika hatua nyingine Machibya Ameiomba halmashauri ya mji wa Kahama kufanya msako na kuwazuia wafanyabiashara wa mifugo kupakia Ng’ombe usiku kwani ng’ombe wengi wa wizi wanasafirishwa nyakati hizo bila kukaguliwa vibali.

Naye diwani wa kata ya Nyandekwa KULWA KADEBE amewataka vijana kujiunga na vikundi vya ujasiliamali ili kuondokana na tabia ya kukaa vijiweni huku diwani wa viti maalumu Cesilia Mpemba akitoa wito kwa wanawake kuwaelimisha watoto kuhusu maadili na kuepuka makundi.

Kata ya Nyandekwa imekumbwa na wizi wa mifugo na Chakula katika siku za hivi karibuni ambapo kati ya mwezi wa saba na nane Familia ya Juakali Mashimba imeibiwa magunia 11 ya Mpunga na Ng’ombe 7 huku familia zingine zikiibiwa kuku.
Share:

WAFANYABIASHARA WA SANGO WILAYANI KAHAMA WAIOMBA HALMASHAURI KUREKEBISHA MIUNDOMBINU YA SOKO HILO


Na Leah Samson 
KAHAMA

Wafanyabiashara katika eneo la Fantom Mjini KAHAMA wameiomba Halmashauri ya Mji huo kuboresha miundombinu ya soko la Sango kabla ya kuwahamishia katika soko hilo ili kuwawezesha kufanya biashara vizuri na usalama wa mali zao.

Hayo yamesemwa jana na Mwenyekiti wa Wafanyabishara katika eneo hilo, RASHID ATHUMAN, na ABASI SHABANI ambaye ni mfanyabiashara walipokua wakizungumza na kahama FM baada ya kupokea agizo la kuhamia katika Soko la Sango.

Kwa upande wake afisa mtendaji wa eneo hilo, INNOCENT KAPELE amesema ofisi Halmashauri inaendelea na taratibu ya kurekebisha miundombinu ya soko hilo ili kuwa na miundombinu rafiki ikiwa ni pamoja na kudhibiti maji yasiingie.

Amesema ni vyema wafanyabiashara hao wahame katika eneo hilo kwani mazingira si salama kwa kuwa wapo barabarani na hakuna vyoo wakati serikali ikiendelea kurekebisha eneo la Sango.
Share:

JESHI LA POLISI JIJINI DODOMA LAKAMATA WATUHUMIWA AKIWEMO CHIDI BENZI

Image result for kamanda mkuu dodoma
Na Lilian
DODOMA

Jeshi la polisi Mkoani DODOMA limemtia Mbaroni mtuhumiwa wa kosa la mauji ya mhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma UDOM pamoja na watuhumiwa wengine 7 akiwemo msanii wa muziki wa bongo fleva RASHID ABDALLAH Maarufu CHID BENZI kwa kosa la kujihusisha na biashara haramu.

Akizungumza na waandisha wa habari kamanda wa polisi mkoani Dodoma GILLES MUROTO Amesema jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa aliyehusika na mauji ya Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma UDOM ROSE MALFRED MDENYE na mume wake JOHN MWAISAGO yaliyotokea tarehe 25.05.2018 swaswa mtaa wa sulungai na mtuhumiwa huyo kutororka.

Mtuhumiwa huyo ametiwa baroni akiwa mafichoni katika kijiji cha chiwachiwa kata ya mbigu wilaya ya ifakara mkoani Mororgoro na atafikishwa mahakamani kwa kosa la kuua kwa kukusudia.

Kupitia operesheni hiyo ya jeshi la polisi msanii wa mziki wa bongo fleva ABDALLAH RASHID (33) Maarufu kama CHID BENZ amekamatwa akiwa na Bhagi gram 5 katika msokoto ambayo ni kinyume cha sheria na mtuhumiwa huyo atafikishwa tena mahakamani kwa kosa jipya.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine saba 7 katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Tanzania wakijihusisha na biashara haramu ya wanyamapori ambao ni kombe 536 ikiwa ni kinyume cha sheria.

Kwa upande wake afisa wanyamapori mkoa wa Dodoma SLIVANUS OKUDO mewaomba wananchi kufikisha taarifa pindi wanapoona wahujumu wa maliasili na kupeleka nje ya nchi ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

Jeshi la polisi limewatahadharisha wananchi kuacha kujihusisha na masuala ya uhalifu kwani mkondo wa sheria utafanya kazi yake
Share:

BAADHI YA WANANCHI WA KAHAMA WATOA MAONI YAO JUU YA BAJETI INAYOENDELEA KUJADILIWA BUNGENI DODOMA

Image result for bajeti ya tanzania 2018/19
Na Leah Samson
KAHAMA.

Baadhi ya wananachi Wilayani KAHAMA Mkoani SHINYANGA wamesema bajeti ya fedha ya mwaka 2018/2019 inayoendelea kujadiliwa bungeni Mjini Dodoma, huenda ikatoa fursa ya maendeleo kwa wananchi na taifa kutokana na kuwa imegusa maisha ya Watanzania walio wengi.

Wakizungumza na Kahama fm, wananachi hao wamesema wameipokea vizuri bajeti hiyo iliyowasilishwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Waziri wa Fedha na Mipaango Dokta PHILIPH MPANGO hasa katika suala la kutokuongeza kodi kwenye bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi.

Katika hatua nyingine wananchi hao pia wametoa wito kwa serikali kuongeza bajeti ya kilimo kwani asilimia kubwa ya wanchi nchini wanategemea sekta hiyo katika kujiimarisha kiuchumi.
Share:

WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUINGIA IFADHINI KINYUME CHA SHERIA.

Image result for nyundo mahakamani
Na Paulina juma
KAHAMA.

Wakazi watatu wa kijijini cha MTAKUJA na mmoja mkazi wa NYANTAKARA wilaya ya Bukombe mkoani Geita wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama kwa tuhuma ya kuingia katika hifadhi ya pori la Moyowosi Kigosi kinyume cha sheria.

Waliofikishwa mahakamani ni pamoja na YUSUPH DANIEL (58), ISURURU KAGEMBE (64), NTEMI MASASILA (36) na SAFARI LUCAS (21) mkazi wa Nyantakara Bukombe mkoani Geita.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo USHINDI SWALLO mwendesha mashitaka wa Idara ya wanyama pori CATHELINE ALOYCE amesema washitakiwa walitenda kosa hilo June 15 mwaka huu majira ya saa 11 jioni ambapo waliingia ndani ya hifadhi bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori.

CATHELINE amesema washitakiwa hao pia waliharibu uoto wa asili ndani ya hifadhi hiyo kwa kukata miti kwa ajili ya mbao bila kibali kutoka kwa mkurungezi wa wa wanyamapori.

Katika shauri hilo la jinai namba 223/2018 Washitakiwa wote wamekili kutenda kosa la kuingia hifadhi kinyume na kifungu namba 15 cha sheria ya uhifadhi wanyama pori namba 5 ya mwaka 2009.

Hata hivyo hoja za msingi zitasomwa Mahakamani hapo June 29 mwaka huu na watumiwa wote wamerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
Share:

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA YA KUMSABABISHIA UJAUZITO MWANAFUNZI


Na Lilian Katabaro
KAHAMA.

Mkazi wa kijiji cha Ufala Wilayani KAHAMA, JOSHUA ANDREW amefikishwa katika mahakama ya Wilaya hiyo kwa tuhuma ya kubaka na kumsababishia ujauzito mwanafunzi wa miaka 16 kinyume na sheria.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, USHINDI SWALLO, Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi, FELIX MBISE amesema ANDREW alitenda kosa May 31 mwaka huu saa 2 asubuhi katika kijiji cha Ufala ambapo alimbaka mwanafunzi huyo na kumsababishia ujauzito.

FELIX amesema katika shauri hilo la jinai namba 215/2018 ANDREW anatuhumiwa kwa kosa la kwanza la kubaka kinyume na kifungu 130 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Amesema kosa la pili, ANDREW anatuhumiwa kumsababishia mwanafunzi ujauzito kinyume na kifungu namba 60 A cha sheria ya elimu sura ya 353 kanuni ya adhabu ya mwaka 2016.

ANDREW amekana kutenda kosa hilo na upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na shauri hilo litatajwa tena mahakamani hapo June 23 mwaka huu na amerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
Share:

MBUNGE WA ZAMANI WA JIMBO LA KAHAMA JAMES LEMBELI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JUMATANO



KAHAMA.

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuanzia mwaka 2005 hadi 2015, JAMES LEMBELI, siku ya Jumatano atazungumza na Vyombo vya Habari nyumbani kwake kijijini Mseki Bulungwa wilayani Kahama.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Msaidizi wake, MIPAWA NG’WANANGOLELWA jana, katika mkutano huo LEMBELI ataelezea ushiriki wake katika ujenzi wa taifa na mustakabali wake katika masuala ya kisiasa.

NG'WANANGOLELWA amesema, LEMBELI ambaye katika kipindi chake cha ubunge alipata umaarufu katika mapambano dhidi ya ufisadi nchini, ameamua kuzungumza na vyombo vya habari baada ya ukimya wa muda mrefu.

Kabla ya kujiunga na siasa mwaka 2005, LEMBELI amewahi kufanya kazi katika taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na iliyokuwa Jumuiya ya WASHIRIKA, gazeti la Kiongozi, Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (DW) jijini Berlin na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Katika hatua nyingine, Waislamu nchini wameombwa kuwaombea viongozi wa Taifa la Tanzania bila kujali itikadi zao ili kuleta amani na kuwafanya viongozi wawe na Heshima na Busara katika kuongoza Watanzania na Taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa jana na Mkurugenzi wa Kahama Fm JAMES LEMBELI wakati wa futari aliyoiandaa kwaajili ya waumini wa msikiti wa kijiji cha Iboja kata ya Ukune Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.

Amesema, viongozi wa kiroho katika hali ya kawaida wapo karibu na Mungu hivyo, maombi yao yatafika kwa urahisi kwake mwenyezi Mungu ambaye atashusha neema ya hekima kwa viongozi wa taifa letu na hivyo amani ya nchi yetu kutamalaki.

Ameongeza kuwa kwa kuwa mfungo mtukufu wa Ramadhani ni utekelezaji wa nguzo tano za Uislamu ikiwa ni pamoja na kusali,basi viongozi na waumini kwa ujumla wana wajibu wa kuliombea Taifa letu lizidi kudumisha amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Kwa upande wake, Sheikh wa Msikiti wa Kijiji cha Iboja, ATHUMANI MOHAMED amemshukuru LEMBELI kwa moyo wa upendo na ukarimu na kuongeza kuwa LEMBELI kila mwaka amekuwa na utaratibu wa Kuwafuturisha Waislamu wasio na uwezo na kutoa wito kwa watu wengine wenye uwezo kuiga mfano wake.
Share:

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI


Na Paulina Juma
KAHAMA.

Mkazi wa kijiji cha Mwabomba Kitongoji cha Bukindwasali Wilayani KAHAMA, YOHANA MASANJA (19 amefikiswa katika mahakama ya wilaya hiyo kwa tuhuma ya kumuua LETICIA NDAKI, mkazi wa kijiji hicho cha Mwabomba kinyume na sheria.

Akisoma shitaka hilo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo USHINDI SWALLO, mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi, PETER MASAU amesema MASANJA alitenda kosa hilo May 30 mwaka huu saa 5 asubuhi huko Mwabomba Kitongoji cha Bukindwasali wilayani Kahama.

MASAU amesema MASANJA ametenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo 2002.

Katika shauri hilo la jinai namba 17/2018 MASANJA hakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo limeahirishwa hadi June 25 mwaka huu litakapotajwa mahakamani hapo na amerudishwa rumande kwa kuwa kesi hiyo haina dhamana.
Share:

KAHAMA FM KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MISITU WAPANDA MITI 300 SHULE YA MSINGI NYAHANGA A NA MBULU


Na Samwel Nyahongo
KAHAMA.

Ukosefu wa elimu juu ya umuhimu wa upandaji miti kwa ajili ya uhifadhi wa Mazingira miongoni mwa wakazi wa wilaya ya KAHAMA Mkoani SHINYANGA imekua ni changamoto na kusababisha baadhi ya maeneo wilayani humo kukabiliwa na hatari ya kuwa jangwa.

Hayo yamesemwa na Mmoja wa Wadau wa Maendeleo wilayani humo, Bibi ASHA MSANGI (NAKYOO), katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani uliofanyika katika Shule za Msingi Nyahanga “A” na Mbulu mjini Kahama.

SANJARI na kuhimiza elimu ya mazingira kwa Wananchi, MSANGI amesema vyombo vya dola havina budi kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha vitendo vyovyote vya uharibifu wa mazingira vinakomeshwa wilayani humo na katika taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo BERNADETHA MLWANGWA ameishukuru Kahama fm pamoja na wadau wote walioshiriki kwa kuiona shule hiyo kwani changamoto ya kukosekana kwa miti katika shule yake ni kubwa.

Amewahakikishia Wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa kampeni hiyo wakiwemo Wawakilishi wa Wakala wa Misitu nchini (TFS), Umoja wa Wapanda Miti Kahama na Chama Kikuu cha Ushirika Wilaya ya Kahama (KAKU), kwamba watahakikisha miti yote iliyopandwa inatunzwa na kukua.

Katika hatua nyingine MLWANGWA ameiomba mamlaka ya mji safi na usafi wa mazingira mjini Kahama (KUWASA) kuwapunguzia bei ya bili ya maji ili waweze kupata unafuu katika umwagiliaji wa miti hiyo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nyahanga MICHAEL MAGILE amewaomba wananchi kutunza mazingira na kuacha kuharibu miundombinu hali ambayo itapunguza magonjwa ikiwemo magonjwa ya mlipuko.

Jumla ya miti 300 inatarajiwa kupandwa katika shule hizo za Msingi za Nyahanga “A” na Mbulu katika maadhimisho hayo ya Siku ya Mazingira Duniani nchini ya kampeni hiyo yenye kauli mbiu isemayo: OTESHA MITI-KAHAMA YA KIJANI INAWEZEKANA.

Siku ya Mazingira Duniani huadhimishwa kila Juni Tano ya kila Mwaka ambapo kimataifa kauli mbiu yake inasema: TOKOMEZA UCHAFUZIWA MAZINGIRA UNAOSABABISHWA NA MIFUKO MICHAFU YA PLASTIKI.

Kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam ambapo kaulimbiu ya kitaifa ni MKAA UNA GHARAMA, TUMIA NISHATI MBADALA.
Share:

WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUINGIA PORI LA AKIBA LA KIGOSI MOYOWOSI KINYUME CHA SHERIA


Na Lilian Katabaro
KAHAMA.

Wakazi wa kijijini cha Kilimahewa wilayani Kahama EZEKIEL CHARLES (52) na REVOKATUS MAGANGA (36) wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya hiyo kwa tuhuma za kuingia katika Pori la Akiba la Moyowosi-Kigosi na kupatikana na mchanga wenye madini bila kibali.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo IMANI BATENZI, mwendesha mashitaka wa Idara ya wanyama pori CATHERINE ALOYCE amesema washitakiwa walitenda kosa hilo Mei 30 mwaka huu majira ya saa nne usiku kwa kuingia ndani ya hifadhi bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori.

CATHERINE amesema katika shitaka la pili washitakiwa hao pia walikamatwa wakiwa na mchanga unaosadikika kuwa na madini ya dhahabu viroba vinne kinyume na kifungu namba 20 cha sheria ya uhifadhi wanyama pori ya mwaka 2009.

Katika shauri hilo la jinai namba 206/2018 Washitakiwa wamekiri kuingia katika Pori hilo la Akiba Moyowosi-Kigosi kinyume na kifungu namba 15 cha sheria ya uhifadhi wa wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.

Kosa la pili ni kupatikana na mchanga unaodhaniwa unamadini ya dhahabu kinyume na kifungu namba 20 cha sheria ya uhifadhi wanyamapori ya mwaka 2009.

Kufuatia hatua ya Washitakiwa kukiri makosa hayo, hoja za msingi zitasomwa Mahakamani hapo June 14 mwaka huu na watuhumiwa wote wamerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
Share:

ZAIDI YA WANAUME 35,000 MKOA WA SHINYANGA WAFANYIWA TOHARA


Na Sebastian Mnakaya
KAHAMA.

Zaidi ya wanaume 35,000 katika mkoa wa SHINYANGA wamefanyiwa tohara katika vituo mbalimbali mkoani humo katika kipindi cha Octoba mwaka jana hadi mwezi Machi mwaka huu, huku ikitarajiwa kuwafanyia wanaume 64,000 ifikapo Septemba mwaka huu.

Akizungumza leo na KAHAMA FM mshauri wa huduma za tohara kwa wanaume kutoka shirika la INTRAHEALTH INTERNATIONAL mkoani Shinyanga, Dkt ENNOCENT MBUGI amesema zoezi hilo linawalenga watoto kuanzia umri wa miaka 10 na watu wazima.

Naye mtoa huduma za tohara kwa wanaume katika hospitali ya Halmashauri ya mji wa Kahama, LINDA KIDOLEZI amesema kumekuwa na muitikio mdogo miongongoni mwa wanaume wenye umri kuanzia miakaa 20 na kuendelea ikilinganishwa na wale wa chini ya umri huo.

Kwa upande wao baadhi ya Wanaume waliofanyiwa tohara katika Hospitali ya mji wa Kahama wamesema wanajisikia fahari na kujiamini baada ya zoezi hilo kwani wana uhakika wa kuepuka maambukizi ya magonjwa ya ngono ukiwemo UKIMWI kwa asilimia kubwa.

Serikali kwa kushirikiana na Shirika la INTRAHEALTH INTERNATIONAL mwaka 2010 ilianzisha kampeni hiyo ya tohara bure kwa wanaume kuanzia miaka kumi hadi miaka 60, lengo likiwa ni kuwaepusha na uwezekano wa kuambukizana magonjwa ya ngono, hususan UKIMWI.
Share:

WATU WANNE WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAUAWA NA POLISI


Na Salvatory Ntandu
KAHAMA.

Watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuawa katika majibizano ya risasi baina yao na askari polisi katika Makaburi ya Kitwana wilayani Kahama, huku silaha nne za kivita na bomu moja la kutupa kwa mkono vikipatikana katika tukio hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mjini Kahama Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, SIMON HAULE amesema tukio limetokea jana majira ya saa sita mchana baada ya watuhumiwa hao kutaka kuwakimbia polisi waliokuwa wanawashikilia.

Amesema watu hao walikamatwa na Jeshi la Polisi katika mikoa ya Tabora, Katavi, Shinyanga na Kigoma ambapo walitoa ushirikano kwa jeshi la Polisi na kuonesha Mahali ambapo huwa wanaficha silaha hizo katika eneo la Makaburi ya Kitwana.

Naye Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Shinyanga aliyeendesha msako huo, AMADIUS TESHA amewataka Majambazi popote walipo kusalimisha silaha zao na wasipofanya hivyo hawatasalimika.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kitwana wamelipongeza jeshi la Polisi kufanikisha msako huo ambao umewezesha kukamatwa kwa silaha hizo.

Silaha zilizokamatwa ni pamoja na bunduki aina ya AK47 yenye risasi 30, Shotgun 1, Bastola 2 zenye risasi na Bomu moja la kutupa kwa mkono.
Share:

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels